Na Fadhili Abdallah,Kigoma
wazazi na wananchi wa
maeneo mbalimbali ya halmashauri ya wilaya kigoma wametakiwa kuwapokea na
kuwatendea vizuri walimu wapya wanaopangwa kufundisha katika shule za msingi na
sekondari ili kuwafanya walimu hao wasikimbie vituo vyao vya kazi.
Akizungumza katika shule
ya msingi Nkungwe wakati akikagua maendeleo na mapokezi ya walimu wapya
waliopangwa katika hamlashauri hiyo Afisa elimu shule ya msingi wa halmashauri
ya wilaya Kigoma, Maya Mlangi amesema walimu hao wapya wanapaswa watendewe
vyema ili kuwafanya watulie kwenye vituo vyao.
Mlangi alisema kuwa moja
ya mambo ambayo yalikuwa yakiwakimbiza walimu katika maeneo waliyokuwa
wakipangiwa ni pamoja na mapokezi hafifu kutoka kwa wananchi hao ikiwemo
kufanyiwa vitendo vya kishirikina kwa kulazwa nje ya nyumba walizopanga.
kwa upande wake mwalim
mkuu wa shule hiyo, Alfons meshack amesema kuwa uhaba wa nyumba za walimu
imekuwa changamoto kubwa kwa shule yake.
Alisema kuwa shule hiyo
iliyokuwa na walimu watatu haina nyumba za walimu na kwamba kutokana na tatizo
kubwa la walimu na kupatiwa walimu hao wanne imekuwa faraja kubwa kwa wazazi na
wanafunzi wa shule hiyo.
Mwalimu huyo Mkuu wa
shule ya msingi Nkungwe alisema kuwa kutokana na kupangiwa walimu hao wanne wazazi wameamua kuwahudumia kwa kuwalipia
pango la nyumba kwa miezi mitatu pamoja na kuwanunulia vifaa vya ndani.
Mmoja wa walimu hao,
Sara Beche akizungumza kwa niba ya walimu wenzake alisema kuwa watajitahidi kwa
kadri ya uwezo wao kufanya kazi kwa bidii ili kuinua taaluma na kuleta matokeo
mazuri kwa shule hiyo.
mwisho
No comments:
Post a Comment