Friday, April 12, 2013

UZINDUZI MINARA YA TIGO KASULU



 Mkuu wa wilaya Buhigwe, Charles Gishuli akikata utepe kuzindua matumizi ya mnara wa kampuni ya simu ya mkononi ya Tigo anayeshuhudia (kushoto) ni meneja wa tigo kanda ya ziwa Joseph Mutalemwa.

Meneja wa kampuni ya Tigo kanda ya ziwa Joseph Mutalemwa akizungumza katika uzinduzi wa minara ya kampuni hiyo wilayani Kasulu.(Picha na Fadhili Abdallah)



Na Fadhili Abdallah,Kigoma


KAMPUNI ya simu ya mkononi ya tigo imezindua mpango wa uwekaji wa minara mipya ya mawasiliano ili kuongeza wigo wa huduma zake kufikia wateja hadi wale wa vijijini na kufanya mawasiliano ya kampuni hiyo kupatikana wakati wote.


Meneja wa kanda ya ziwa wa Tigo, Joseph Mutalemwa akizungumza kwa niaba ya Meneja Mkuu wa kampuni hiyo, Diego Guiterez alisema kuwa katika awamu ya kwanza ya mpango huo utaanzia kwa mikoa ya Kigoma, Kagera,Tabora,Mwanza na Mara.


Amesema kuwa katika awamu hiyo jumla ya minara  mipya 300 itajengwa ambapo kati hiyo minara 141 itajengwa kanda ya ziwa huku mkoa kigoma itajengwa jumla ya minara 24 na tayari minara mitatu imeshaanza kufanya katika mradi unaotarajiwa kukamilisha mweze Septemba mwaka huu.


katika hatua nyingine kampuni ya tigo imekabidhi jumla ya vitabu 1000 vya masomo ya sayansi vyenye thamani ya shilingi milini saba kwa shule ya msingi Nyaminkunga wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma ili kukabiliana na upungufu wa vitabu unaoikabili shule hiyo.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi vifaa hivyo iliyoenda sambamba na uzinduzi wa mnara wa mawasiliano mjini Kasulu, Meneja wa Tigo Kanda ya ziwa Joseph Mutalemwa alisema kuwa msaada huo ni sehemu ya mpango mkakati wa kampuni hiyo katika kusaidia huduma  za kijamii.

Alisema kuwa vitabu hivyo 1000 vya masomo ya sayansi kwa darasa la nne hadi la sita vinalenga kuchochea wanafunzi katika shule hiyo kupenda masomo ya sayansi ambayo ndiyo msingi wa mainjinia na madokta.

Akizindua kuanza kwa matumizi ya minara hiyo mipya na kukabidhi vitabu Mkuu wa mkoa kigom, Issa Machibya amewataka wananchi wa mkoa huo kutumia uwepo wa mawasiliano ya simu za mkononi kuboresha shughuli zao za kiuchumi.

Katika hotuba iliyotolewa kwa niaba yake na Mkuu wa wilaya Buhigwe, Charles Gishuli alisema kuwa simu za mkononi zimekuwa na matumizi mengi na muhimu kwa maisha ya kila siku ya mwanadamu badala ya kuishia kupiga simu na kutuma ujumbe mfupi wa maandishi.

Mwisho.

No comments:

Post a Comment