Na Mwandishi Wetu, Kigoma.
zaidi ya miche elfu mbili ya bangi
imegundulika na kuteketezwa , ikilimwa katika eneo la msitu wa hifadhi
ya taifa ya akiba ya muyowosi kigosi na maeneo jirani katika wilaya ya
kibondo mkoani kigoma .
hali hiyo imegundulika wakati wa oparesheni maalum ya kusaka mashamba ya bangi iliyofanywa
na jeshi la polisi wakiongozwa na kamanda wa polisi mkoa wa kigoma
fraisser kashai na mkuu wa wilaya ya kibondo venance mwamoto katika
hifadhi hiyo na vijiji vya kagoti, kumhasha na nduta ambapo kamanda
kashai amesema jeshi la polisi litawasaka wamiliki wa mashamba hayo
ambao walikimbia ili wafikishwe mahakamani.
Amesema watu wote waliokimbia
watasakwa na kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayowakabili ambapo
amesema oparesheni hiyo sasa ni endelevu na kwamba wameshapewa taarifa
na raia wema juu ya uwepo wa mashamba zaidi ya bangi katika maeneo
tofauti wilayani humo.
kwa upande wake mkuu wa wilaya ya kibondo venance mwamoto amesema kilimo
cha bangi wilayani humo kimeshamiri na kwamba imekuwa ikisafirishwa
kwenda nchi jirani na mikoa mingine na hivyo kuongeza matumizi ya madawa
ya kulevya katika jamii kinyume cha sheria .
Mwamoto amesema karibu asilimia
sabini ya mashamba ya mazao mbalimbali yanayolimwa wilayani humo
yanachanganywa na bangi hali ambayo inakuwa ngumu lakini watafanya
oparesheni hiyo katika maneo yote na kuwakamata wahusika na kuwachukulia
hatua za kisheria .
Kutokana
na hiyo amewataka viongozi wa hifadhi ya Muyowosi kushughulikia ulinzi
wa hifadhi hiyo ambao sasa umegeuzwa kuwa mashamba ya bangi ili kwa
pamoja waweze kudhibiti kilimo cha bangi wilayani humo.
oparesheni hiyo pia iliwezesha
kukamatwa kwa raia wanane wa burundi ambao walikutwa mashambani
wakifanya kazi za vibarua , wakiwa wameingia nchini , kuishi na kufanya
kazi kinyume cha sheria .
Kaimu afisa uhamiaji wa wilaya ya
Kibondo Rogert Mbele amesema wilaya hiyo ina wahamiaji wengi toka nchi
jirani ya Burndi ambao wamekuwa wakiingia nchini na kuishi vijijini huku
wakifanya kazi za vibarua mashambani .
Amesema hali hiyo inatokana na
ukubwa wa mpaka na udhibiti mdogo uliopo katika eneo hilo la mpaka na
kwamba hali hiyo inachangiwa na raia wan chi hiyo kuyafahamu zaidi
mazingira ya Kigoma kutokana na kuishi kama wakimbizi kwa miaka kadhaa
nchini .
Mwisho
No comments:
Post a Comment