Mkuu wa wilaya Buhigwe, Charles Gishuli akikata utepe kuzindua matumizi ya mnara wa kampuni ya simu ya mkononi ya Tigo anayeshuhudia (kushoto) ni meneja wa tigo kanda ya ziwa Joseph Mutalemwa.
Meneja wa kampuni ya Tigo kanda ya ziwa Joseph Mutalemwa akizungumza katika uzinduzi wa minara ya kampuni hiyo wilayani Kasulu.(Picha na Fadhili Abdallah)
Na Fadhili
Abdallah,Kigoma
KAMPUNI ya
simu ya mkononi ya tigo imezindua mpango wa uwekaji wa
minara mipya ya mawasiliano ili kuongeza wigo wa huduma zake kufikia wateja
hadi wale wa vijijini na kufanya mawasiliano ya kampuni hiyo kupatikana wakati
wote.
Meneja wa
kanda ya ziwa wa Tigo, Joseph Mutalemwa akizungumza kwa niaba ya Meneja Mkuu wa
kampuni hiyo, Diego Guiterez alisema kuwa katika awamu ya kwanza ya mpango huo
utaanzia kwa mikoa ya Kigoma, Kagera,Tabora,Mwanza na Mara.
Amesema kuwa
katika awamu hiyo jumla ya minara mipya 300 itajengwa ambapo kati hiyo minara 141 itajengwa kanda ya ziwa huku mkoa
kigoma itajengwa jumla ya minara 24 na tayari minara mitatu imeshaanza kufanya
katika mradi unaotarajiwa kukamilisha mweze Septemba mwaka huu.
katika hatua nyingine kampuni ya tigo imekabidhi jumla ya vitabu 1000 vya masomo ya sayansi vyenye thamani ya shilingi milini saba kwa shule ya msingi Nyaminkunga wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma ili kukabiliana na upungufu wa vitabu unaoikabili shule hiyo.
Akizungumza katika
hafla ya kukabidhi vifaa hivyo iliyoenda sambamba na uzinduzi wa mnara wa
mawasiliano mjini Kasulu, Meneja wa Tigo Kanda ya ziwa Joseph Mutalemwa alisema
kuwa msaada huo ni sehemu ya mpango mkakati wa kampuni hiyo katika kusaidia
huduma za kijamii.
Alisema kuwa
vitabu hivyo 1000 vya masomo ya sayansi kwa darasa la nne hadi la sita
vinalenga kuchochea wanafunzi katika shule hiyo kupenda masomo ya sayansi
ambayo ndiyo msingi wa mainjinia na madokta.
Akizindua
kuanza kwa matumizi ya minara hiyo mipya na kukabidhi vitabu Mkuu wa mkoa
kigom, Issa Machibya amewataka wananchi wa mkoa huo kutumia uwepo wa
mawasiliano ya simu za mkononi kuboresha shughuli zao za kiuchumi.
Katika hotuba
iliyotolewa kwa niaba yake na Mkuu wa wilaya Buhigwe, Charles Gishuli alisema
kuwa simu za mkononi zimekuwa na matumizi mengi na muhimu kwa maisha ya kila
siku ya mwanadamu badala ya kuishia kupiga simu na kutuma ujumbe mfupi wa
maandishi.
Mwisho.