Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA,Witness Shoo amesema hayo wakati akizungumza na
waandishi wa habari kutoka klabu ya waandishi wa habari wa Kigoma wanaofanya
ziara ya mafunzo kutembelea hifadhi mbalimbali nchini.
Shoo alisema
kuwa kuendelea kuuawa kwa tembo na faru kunatishia kutoweka kwa wanyama hao
ambao wamekuwa na mchango mkubwa katika sekta ya utalii kutokana na idadi kubwa
ya watalii wanaotembelea hifadhi mbalimbali nchini kuwa na shauku ya kuwaona
wanyama hao.
Katika
kukabiliana na changamoto hiyo Mkurugenzi huyo wa TANAPA amewaomba waandishi wa
habari kutumia vyombo vyao katika kufichua na kuandika bila woga kuhusiana na
ujangiri na kuwatangaza majangiri wanaokamatwa.
Sambamba na
kuandika na kufichua masuala ya ujangiri Shoo amewataka waandishi wa habari
kuandika kwa wingi na kuhamasisha jamii ya Watanzania umuhimu wa kutembelea
hifadhi zetu.
Kwa upande
wake Afisa Habari wa TANAPA, Pascal Shelutete amesema kuwa waandishi wa habari
wamekuwa na mchango mkubwa katika kukuza na kuendeleza sekta ya utalii hasa
katika kuvitangaza vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo nchini.
Shelutete
alisema kuwa mchango wa waandishi wa habari umekuwa na faida kubwa na umechangia
kuongeza idadi ya Watanzania kama watalii wa ndani kutembelea hifadhi
mbalimbali nchini.
Mwisho.
Mhifadhi Utalii katika hifadhi ya Taifa ya Arusha Sakinoi mwenye jaketi akieleza namna nyati alivyouawa kwa mitego ya waya kunakofanywa na majangiri
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA witness Shoo (kushoto) akizungumza na waandisha wa habari kutoka Kigoma Press Club waliokuwa wakifanya ziara ya utalii wa ndani kutembelea hifadhi mbalimbali nchini hapa ni makao makuu ya TANAPA mjini Arusha.
(Picha na Fadhili Abdallah)
No comments:
Post a Comment