Wednesday, June 25, 2014



                        MTO MAGARA WAHITAJI UJENZI WA DARAJA
Wakiendelea na utalii wa ndani uliodhaminiwa na mamlaka ya hifadhi nchini Tanzania (TANAPA), waandishi wa habari wa mkoa wa Kigoma wamebaini kuwa kuna tatizo la ujenzi wa daraja la mto Magara unaokwamisha baadhi ya shughuli za maendeleo  hasa wakati wa masika.

Wakiongea na baadhi ya wananchi waliopo katika  kata ya  Magara Wilayani Babati Mkoani Arusha wananchi hao wamezungumzia  madhara  wanayo yapata wakati wa masika kutokana na mafuliko makubwa  ambayo yanajitokeza kila mwaka katika mto huo wa Magara.


Mmoja wao Bw. Muhidin Said amesema wakati wa masika wakulima hushindwa kuendesha shughuli zao  za kilimo  na wakati mwingime mazao yote kusombwa na  maji jambo ambalo husababisha hasara kubwa kwa wakulima.

Naye Bw. Edward  Mariko  amesema katika msimu wa kilimo wa mwaka 2011/2013 zaidi ya nyumba nne zilivunjwa na watu watatu walipoteza maisha kutokana na mafuriko na kusisitiza  kuwa  maji yanapo jaa katika mto huo shughuli zote za maendeleo husitishwa mpaka maji yapundue hivyo ujenzi wa daraja hilo ni muhimu kwa maendeleo yao.

Zaidi wananchi hao walisema kuwa kwa kipindi cha masika kumekuwa na ukwamishaji wa masoma kwa wanafunzi wanotoka katika vijiji vya pembezoni mwa mto na kuwafanya wakose masoma yanyokuwa yanaendelea kwa wakati huo, au kuwafanya wachelewe darasani kwani huwa inawalazimu kusubiri mpaka maji yapungue .

Kwa upande wake Afisa Muhifadhi wa Utalii kutoka Hifadhi ya taifa ya Manyara Bw. Ibrahimu Mtui amesema shughuli nyingi za utalii zimekwama katika eneo hilo la Magarama kutokana na watalii kushindwa kutumia barabara hiyo  kuingia ndani ya hifadhi kwa kuhofia usalama wao.

Mwisho

No comments:

Post a Comment