Miti ni kati ya vivutio vikubwa vya asili
tulivyonavyo hapa nchini Tanzania,miti ni maliasili, miti ni uhai.
Huleta hali nzuri ya hewa, husababisha mvua
kunyesha, huleta kivulu, na hulinda vyanzo vya maji. Haya ni kati ya mambo
muhimu ambayo miti husaidia katika upatikanaji wake, je, itakuwaje siku ambapo
rasilimali hii muhimu itatoweka?
“Ole Africana” kwa jina maarufu Msenefu, ni kati ya
miti inayopatikana katika Hifadhi ya Taifa ya Arusha, mti huu unakamata nafasi
ya pili kwa ugumu baada ya mpingo na sifa nyingine za mti huu ni kwamba
haubunguliwi, wala hailiwi na mchwa, na uhai wake ni zaidi ya miaka 100
duniani, mti huu haukuwi kwa haraka na wala haina umbile kubwa.
Akiongea katika Hifadhi yaTaifa ya Arusha muhifadhi
bwana Samweli Sakinoi, ambaye ni Afisa Utalii katika hifadhi hiyo amesema kuwa
kutokana na ubora na ugumu wa miti hiyo
imekuwa ikitumika katika shughuli mbalimbalimiti ambazo ndizo
zinapelekea chanzo cha miti hiyo kutoweka.
Mti huo umekuwa ukitumika katika shughuli za
ujenzi, hasa ujenzi wa choo pamoja na kutungika kwenye paa kama kenchi, zaidi
miti hiyo imekuwa ikitumika kwaajili ya kusafishia vibuyu vinavyotumika
kugandishia maziwa ambayo baadae hufanya maziwa hayo kuwa na radha nzuri.
Hizo ni kati ya sababu ambayo zinazoweza kusababisha
mti huu kutoweka kabisa, lakini zipo sababu nyingine ambazo husababisha miti
zaidi kupotea na kutoweka kabisa katika Sayari Dunia.
Sababu hizi ni pamoja na kukata miti ovyo kwaajili
ya kutengeneza mbao, kuchoma misitu kwaajili ya malisho ya mifugo, biashara za
mgogo kwaajili ya kufyatulia tofari na ukaushaji tumbaku, hii hutokea zaidi
katika mikoa ya Kigoma na Tabora.
Hata hivyo bwana Sakinoi amesema kuwa Hifadhi ya Taifa
ya Arusha imekuwa ikitoa elimu juu ya tunzaji wa mazingira na kuwa wananchi
wanaweza wakafanya shughuli nyingine za kujipatia kipato kuliko kutumia rasilimali
miti na kuzitumia kwa shughuli za utafutaji jambo ambalo utafanya baadhi ya
miti muhimu kupotea.
Zaidi Afisa Utalii huyo ametoa rai kuwa kwakuwa
mbegu za miti hiyo zinapatikana wananchi hawana budi kupanda miti hiyo kwa wingi, ili kuepuka
utokomeaji wake.
Mwisho
Adela Madyane.
No comments:
Post a Comment