Thursday, June 26, 2014




Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA,Witness Shoo amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kutoka klabu ya waandishi wa habari wa Kigoma wanaofanya ziara ya mafunzo kutembelea hifadhi mbalimbali nchini.

Shoo alisema kuwa kuendelea kuuawa kwa tembo na faru kunatishia kutoweka kwa wanyama hao ambao wamekuwa na mchango mkubwa katika sekta ya utalii kutokana na idadi kubwa ya watalii wanaotembelea hifadhi mbalimbali nchini kuwa na shauku ya kuwaona wanyama hao.

Katika kukabiliana na changamoto hiyo Mkurugenzi huyo wa TANAPA amewaomba waandishi wa habari kutumia vyombo vyao katika kufichua na kuandika bila woga kuhusiana na ujangiri na kuwatangaza majangiri wanaokamatwa.

Sambamba na kuandika na kufichua masuala ya ujangiri Shoo amewataka waandishi wa habari kuandika kwa wingi na kuhamasisha jamii ya Watanzania umuhimu wa kutembelea hifadhi zetu.

Kwa upande wake Afisa Habari wa TANAPA, Pascal Shelutete amesema kuwa waandishi wa habari wamekuwa na mchango mkubwa katika kukuza na kuendeleza sekta ya utalii hasa katika kuvitangaza vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo nchini.

Shelutete alisema kuwa mchango wa waandishi wa habari umekuwa na faida kubwa na umechangia kuongeza idadi ya Watanzania kama watalii wa ndani kutembelea hifadhi mbalimbali nchini.

Mwisho.



 

Mhifadhi Utalii katika hifadhi ya Taifa ya Arusha  Sakinoi mwenye jaketi akieleza namna nyati alivyouawa kwa mitego ya waya kunakofanywa na majangiri


Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA witness Shoo (kushoto) akizungumza na waandisha wa habari kutoka Kigoma Press Club waliokuwa wakifanya ziara ya utalii wa ndani kutembelea hifadhi mbalimbali nchini hapa ni makao makuu ya TANAPA mjini Arusha.

(Picha na Fadhili Abdallah)

Wednesday, June 25, 2014



                        MTO MAGARA WAHITAJI UJENZI WA DARAJA
Wakiendelea na utalii wa ndani uliodhaminiwa na mamlaka ya hifadhi nchini Tanzania (TANAPA), waandishi wa habari wa mkoa wa Kigoma wamebaini kuwa kuna tatizo la ujenzi wa daraja la mto Magara unaokwamisha baadhi ya shughuli za maendeleo  hasa wakati wa masika.

Wakiongea na baadhi ya wananchi waliopo katika  kata ya  Magara Wilayani Babati Mkoani Arusha wananchi hao wamezungumzia  madhara  wanayo yapata wakati wa masika kutokana na mafuliko makubwa  ambayo yanajitokeza kila mwaka katika mto huo wa Magara.


Mmoja wao Bw. Muhidin Said amesema wakati wa masika wakulima hushindwa kuendesha shughuli zao  za kilimo  na wakati mwingime mazao yote kusombwa na  maji jambo ambalo husababisha hasara kubwa kwa wakulima.

Naye Bw. Edward  Mariko  amesema katika msimu wa kilimo wa mwaka 2011/2013 zaidi ya nyumba nne zilivunjwa na watu watatu walipoteza maisha kutokana na mafuriko na kusisitiza  kuwa  maji yanapo jaa katika mto huo shughuli zote za maendeleo husitishwa mpaka maji yapundue hivyo ujenzi wa daraja hilo ni muhimu kwa maendeleo yao.

Zaidi wananchi hao walisema kuwa kwa kipindi cha masika kumekuwa na ukwamishaji wa masoma kwa wanafunzi wanotoka katika vijiji vya pembezoni mwa mto na kuwafanya wakose masoma yanyokuwa yanaendelea kwa wakati huo, au kuwafanya wachelewe darasani kwani huwa inawalazimu kusubiri mpaka maji yapungue .

Kwa upande wake Afisa Muhifadhi wa Utalii kutoka Hifadhi ya taifa ya Manyara Bw. Ibrahimu Mtui amesema shughuli nyingi za utalii zimekwama katika eneo hilo la Magarama kutokana na watalii kushindwa kutumia barabara hiyo  kuingia ndani ya hifadhi kwa kuhofia usalama wao.

Mwisho

Sunday, June 22, 2014

KUTEMBELEA HIFADHI YA ARUSHA UTALII WA NDANI

 Waandishi wa habari kutoka Kigoma Press Club wakipata maelezo kuhusu hifadhi ya Taifa ya Arusha walipofanya ziara ya utalii wa ndani kutembelea hifadhi hiyo waliosimama kulia ni viongozi wa hifadhi ya Taifa ya Arusha

MTI YA MSENEFU HATARINI KUTOWEKA.



Miti ni kati ya vivutio vikubwa vya asili tulivyonavyo hapa nchini Tanzania,miti ni maliasili, miti ni uhai.
 
Huleta hali nzuri ya hewa, husababisha mvua kunyesha, huleta kivulu, na hulinda vyanzo vya maji. Haya ni kati ya mambo muhimu ambayo miti husaidia katika upatikanaji wake, je, itakuwaje siku ambapo rasilimali hii muhimu itatoweka?

“Ole Africana” kwa jina maarufu Msenefu, ni kati ya miti inayopatikana katika Hifadhi ya Taifa ya Arusha, mti huu unakamata nafasi ya pili kwa ugumu baada ya mpingo na sifa nyingine za mti huu ni kwamba haubunguliwi, wala hailiwi na mchwa, na uhai wake ni zaidi ya miaka 100 duniani, mti huu haukuwi kwa haraka na wala haina umbile kubwa.



Akiongea katika Hifadhi yaTaifa ya Arusha muhifadhi bwana Samweli Sakinoi, ambaye ni Afisa Utalii katika hifadhi hiyo amesema kuwa kutokana na ubora na ugumu wa miti hiyo  imekuwa ikitumika katika shughuli mbalimbalimiti ambazo ndizo zinapelekea chanzo cha miti hiyo kutoweka.

Mti huo umekuwa ukitumika katika shughuli za ujenzi, hasa ujenzi wa choo pamoja na kutungika kwenye paa kama kenchi, zaidi miti hiyo imekuwa ikitumika kwaajili ya kusafishia vibuyu vinavyotumika kugandishia maziwa ambayo baadae hufanya maziwa hayo kuwa na radha nzuri.

 Hizo ni kati ya sababu ambayo zinazoweza kusababisha mti huu kutoweka kabisa, lakini zipo sababu nyingine ambazo husababisha miti zaidi kupotea na kutoweka kabisa katika Sayari Dunia.


Sababu hizi ni pamoja na kukata miti ovyo kwaajili ya kutengeneza mbao, kuchoma misitu kwaajili ya malisho ya mifugo, biashara za mgogo kwaajili ya kufyatulia tofari na ukaushaji tumbaku, hii hutokea zaidi katika mikoa ya Kigoma na Tabora.

Hata hivyo bwana Sakinoi amesema kuwa Hifadhi ya Taifa ya Arusha imekuwa ikitoa elimu juu ya tunzaji wa mazingira na kuwa wananchi wanaweza wakafanya shughuli nyingine za kujipatia kipato kuliko kutumia rasilimali miti na kuzitumia kwa shughuli za utafutaji jambo ambalo utafanya baadhi ya miti muhimu kupotea.

Zaidi Afisa Utalii huyo ametoa rai kuwa kwakuwa mbegu za miti hiyo zinapatikana wananchi hawana budi  kupanda miti hiyo kwa wingi, ili kuepuka utokomeaji wake.

Mwisho
Adela Madyane.

Tuesday, June 3, 2014

MAZISHI YA SHIDA SALUM MAMA MZAZI WA ZITTO KABWE




 Naibu Spika wa bunge Job Ndugai (kulia) akiwa katika mazishi ya Mama yake mzazi zitto Kabwe mbunge wa jimbo la kigoma kaskazini Shida Salum yaliyofanyika mjini Kigoma (wa pili Kulia) Mwenyekiti wa CCM mkoa Kigoma Walid Kabourou,wabunge Nimrod Mkono na Ally Kesi.


 Baadhi ya wabunge wa bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania na vyama vya siasa wakiwa na Zitto Kabwe wakielekea makaburi ya Rubengela Mjini Kigoma kwa mazishi


   ZITTO ATOA YA MOYONI MSIBA WA MAMA YAKE


MBUNGE wa jimbo la Kigoma Kaskazini Zitto ameongoza maelfu ya viongozi na wananchi kutoka pande mbalimbali za nchi katika mazishi ya mama yake Mzazi Shida Salum na kutoa agizo kwa Naibu Spika wa Bunge Job Ndugai na Mwenyekiti wa CUF Ibrahimu Lipumba kumuenzi mama yake kwa kuwaletea watanzania katiba mpya wanayoitaka.

Zitto alisema hayo nyumbani kwa Marehemu mama yake mtaa Kisangani mwanga mjini kigoma  muda mfupi kabla ya kuelekea makaburi ya Rubengela mjini Kigoma ambako mwili wa Shida Salum ulizikwa.

Mbunge huyo Kijana alisema kuwa kama kweli viongozi hao wanataka kumuenzi mama yake wamalize tofauti zao na kulifanya bunge la katiba kuendelea na shughuli yake ya kuwaletea Watanzania katiba itakayowafaa kwa muda mrefu.

Alisema kuwa Mama yake alikuwa mjumbe wa bunge hilo la katiba kufuatia kuteuliwa na Raisi Jakaya kikwete jambo ambal lingempa nafasi ya kuandika historia ya kuwa mmoja wa wajumbe wa bunge hilo katika kuandika katiba mpya ya Tanzania.

Zitto alisema kuwa hata hivyo ugonjwa uliokuwa ukimsumbua na mwenyezi mungu kumpitisha kudra zake umeondoa nafasi ya mama yake kuandika historia hiyo na kwamba kilichobaki ni kwa viongozi na wajumbe wa bunge la katiba kufikia maridhiano na kuandika katiba hiyo.

Alisema kuwa amejitahidi kwa kadri ya uwezo wake katika kuhakikisha anamsaidia mama yake kupata mataibabu ambayo yangerudisha afya yake na kumfanya arusi kwenye shughuli zake za kawaida lakini mungu alipitisha maamuzi yake ambayo hakuna wa kuyapinga.

Kwa upande wake Naibu Spika wa bunge la Tangazania,Job ndugai ambaye aliongeza wabunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye mazishi hayo amemuelezea shida Salum kama mtu ambaye alikuwa mtetezi wa watanzania wa hali ya chini.

Hata hivyo Ndugai alisema kuwa Yaliyotokea ni mapenzi ya mungu na kuitaka familia  wasihuzunike kiasi cha kupitiliza wakae pamoja na kuweka familia pamoja na kusonga mbele katika utekelezaji wa majukumu yao ya taifa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taifa wa chama cha wananchi (CUF),Profesa Ibrahimu Lipumba alisema kuwa shida Salum alisimama kuwapigania watu wenye ulemavu mchango ambao alikusudia kuutoa kwenye bunge maalum la Katiba.

Hata hivyo Lipumba alionya kuwa kama kweli watu wanania ya kumuenzi marehemu shida Salum hawana budi kusikiliza maoni ya wananchi walio wengi katika kuipata katiba mpya badala ya watu wachache kutaka kuchakachua.

Naye Mbunge wa jimbo la Kigoma Kusini,David Kafulila alisema kuwa mkoa kigoma umekuwa mkoa wa vyama mbalimbali vya siasa vyenye wabunge kutoka vyama tofauti lakini Mama yake Zitto alikuwa mstari wa mbele katika kuwaunganisha kuwa wamoja kwa ajili ya maslahi ya mkoa Kigoma na watu wake.

na wabunge wa vingawa mkoa kigoma unaonyesha mkoa una mchanganyiko wa vyama mbalimbali vya siasa huyo mama aliwasaidia kuimarisha umoja wao.

Katika mazishi hayo CHADEMA iliwakislishwa na Mbunge wa jimbo la Nyamagana, Ezekie Wenje ambaye alisema kuwa shida Salum alikuwa kiongozi ambaye alisimamia kile anachokiamini wakati wa vikao vya kamati kuu na mikutano mbalimbali ya chadema.

Mazishi hayo pia yalihudhuriwa na Naibu waziri wa Fedha, Adam Malima, Mwenyekiti wa NCCR – Mageuzi, james Mbatia, mbunge wa Kigoma mjini, Peter serukamba, mbunge wa Kasulu mjini, Moses Machali, Mbunge wa Nkasi, ally Kesi, Mbunge wa tabora, Ismail Aden Rage, Mbunge wa Namtumbo, Vita Kawawa.

Aidha pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali na vyama vya siasa  mkoa kigoma ukiwakilishwa na Mkuu wa mkoa,Issa Machibya na Mwenyekiti wa CCM wa mkoa, Walid Aman Kabourou ambapo Mkuu wa mkoa alisema kuwa amefarijika kuona mamia ya watu kutoka pande mbalimbali za nchi hii wakihudhuria mazishi ya mama shida jambo linaloonyesha kwamba alikuwa mtu aliyeishi na watu na kuwa msaada mkubwa kwao.

Mwisho.