Tuesday, February 12, 2013

SIKU YA SHERIA NCHINI


HAKIMU  mkazi mfawidhi wa mkoa Kigoma Emanuel Mrangu (kati kati) akimuongoza Mkuu wa mkoa Kigoma  Issa Machibya (kushoto) kuingia kwenye viwanja vya mahakama ya mkoa Kigoma wakati wa siku ya sheria nchini (kulia) ni Hakimu mkazi mfawidhi wa wilaya kigoma David Ngunyale

KUKATA UTEPE WAKATI WA KUWEKA JIWE LA MSINGI


Raisi Kikwete na wadau wa maendeleo wakikata utepe kuweka jiwe la msingi ujenzi wa uwanja wa ndege wa kigoma

KIKWETE AKIKAGUA AIRPORT YA KIGOMA

Raisi Jakaya kikwete akikagua maendeleo ya upanuzi na uboreshaji wa uwanja wa ndege wa kigoma

Alipata bahati ya kupiga picha ya Pamoja na wadau mbalimbali

WARUMBA NYAKANGA WAKIMKARIBISHA KIKWETE

 kikundi cha ngoma za asili cha Warumba Nyakanga cha mji mdogo wa uvinza wakimkaribisha Raisi kikwete kukagua ujenzi wa Daraja la Malagarasi

Raisi Kikwete akipiga picha ya ukumbusho na mke wake Salma kikwete pembeni ya mto Malagarasi wakati alipofanya ziara kutembelea na kukagua ujenzi wa daraja hilo hapa ni chini ya daraja

KIKWETE AKIKAGUA MRADI WA UJENZI WA DARAJA


 viongozi wa serikali na wadau mbalimbali wa maendeleo wakisikiliza maelezo kuhusu mradi wa ujenzi wa Daraja la Malagarasi (Daraja la kikwete) wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma wakati Raisi Kikwete alipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi ya mradi huo.


Raisi Kikwete akitembelea bonde la mto Malagarasi wakati alipokuwa akikagua mradi wa ujenzi wa daraja la Malagarasi (Daraja la kikwete) alipokuwa kwenye ziara ya siku mbili mkoani Kigoma

RAISI KIKWETE ALIPOZURU DARAJA LA MALAGARASI



 Raisi Jakaya Kikwete akitembelea na kukagua ujenzi wa daraja la Malagarasi wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma alipokuwa kwenye ziara ya siku tatu mkoani Kigoma

Sunday, February 10, 2013

KIKWETE APAMBA MAADHIMISHO MIAKA 36 YA CCM

RAISI JAKAYA KIKWETE AKIHUTUBIA MAMIA YA WAKAZI WA MKOA KIGOMA WAKATI WA KILELE CHA MAADHIMISHO YA MIAKA 36 YA CCM AMBAYO ILIFANYIKA KITAIFA MKOANI KGOMA
 Katibu Mkuu wa CCM Abdullrahman Kinana akizungumza na wananchi wa mkoa kigoma katika maadhimisho hayo.

mamia ya wakazi wa mkoa Kigoma kutoka wilaya zote za mkoa huo wakiwa wamefurika kwa wingi kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 36 ya CCM katika sherhe zilizofanyika kwenye uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.
                             (Picha zote na Fadhili Abdallah)

KILELEL MIAKA 36 YA KUZALIWA CCM

Waziri wa uchukuzi Harrison Mwakyembe akiongea na wananchi wa mkoa kigoma katika kilele cha miaka 36 ya kuzaliwa kwa CCM iliyofanyika kwenye uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.

Saturday, February 9, 2013

MAADHIMISHO MIAKA 36 YA CCM

 Sehemu ya viongozi, wapenzi na wanachama wa CCM wakimsikiliza Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho Jakaya kikwete wakati akitoa neno la kuwashukuru baada ya matembezi ya mshikamano kuadhimisha miaka 36 ya kuzaliwa CCM


Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM Taifa Salma kikwete akiwapungua mkono viongozi,wanachama na wapenzi wa CCM waliohudhuria kilele cha matembezi ya mshikamano ya maadhimisho ya miaka 36 ya kuzaliwa CCm yaliyoishia ofisi kuu ya CCM mkoa kigoma.


mwenyekiti wa Taifa wa CCM Jakaya kikwete akizungumza na wana CCM baada ya kuongoza matembezi ya mshikamano ikiwa sehemu ya maadhimisho ya miaka 36 ya kuzaliwa chama hicho.

MIAKA 36 YA CCM - MATEMBEZI


Katibu wa siasa na uenezi wa CCM Taifa Nape Nnauye akiongoza akiwa mstari wa mbele katika matembezi ya mshikamano ya maadhimisho ya miaka 36 ya kuzaliwa CCM ambayo yaliongozwa na Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho Jakaya kikwete Nyuma ya Nape ni Mkuu wa wilaya kigoma Ramadhani Maneno

Mwenyekiti wa Taifa wa CCM Jakaya kikwete akifurahia ngoma iliyokuwa ikipigwa muda mfupi baada ya kumalizika kwa matembezi ya mshikamano ya miaka 36 ya kuzaliwa kwa CCM yaliyofanyika kitaifa mkoani Kigoma (Picha na Fadhili Abdallah)





MWENYEKITI wa CCM Taifa Jakaya Kikwete amesema kuwa chama hicho kimepania kuhakikisha kwamba mkoa Kigoma unapata maendeleo katika kipindi kifupi kijacho kwa kutekeleza miradi mbalimbali ya wananchi badala ya kukalia maneno na kupiga majungu.

Akizungumza muda mfupi baada ya kumalizika kwa matembezi ya mshikamano ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 36 ya kuzaliwa CCM alisema kuwa wakati huu ni wakati wa kuleta maendeleo mkoa kigoma.

Kikwete ambaye alichukua muda mchache kusalimia wananchi katika ofisi za CCM mkoa kigoma ambapo matembezi hayo ya mshikamano yaliishia alisema kuwa wamepania kwa dhati katika kusimamia jambo.

Alisema kuwa huu si wakati wa blabla na maneno ni wakati wao wanchi wa mkoa kigoma kupata maendeleo na kusisitiza kuwa jambo la muhimu wananchi na viongozi wa mkoa huo kuungana pamoja katika kuhakikisha mipango iliyowekwa ya maendeleo inatekelezwa bila vikwazo.

Awali Mwenyekiti wa CCM mkoa kigoma, Warid Aman Kabourou ameishukuru serikali ya awamu ya nne inayoongozwa na Raisi Jakaya Kikwete kwa kujali na kuonyesha kwa vitendo mkakati wa kuiletea kigoma maendeleo.

Kwa hali ya sasa Kabourou alisema kuwa haina haja ya kumwambia mtu aone kwani kila kitu kinajieleza chenyewe ikiwemo utekelezaji wa miradi mikubwa ya kuimarisha miundo mbinu, miradi ya kiuchumi na miradi ambayo ilikuwa kero kubwa kwa wananchi wa mkoa huo.

Kwa upande wao baadhi ya wanachama wa CCM waandamizi wameeleza kuwa sherehe za miaka 36 ya CCM mkoani Kigoma imekuwa na mafanikio makubwa na hilo linatokana na namna ambavyo wananchi wa mkoa huo walivyoyapokea maadhimisho hayo.

Kotlida Kokupima kutoka wilaya ya Kasulu alisema kuwa majungu, fitina na migogoro baina ya viongozi wa chama hicho imechangia kupunguza mvuto wa chama kwa wananchi na kuchangia kwa viongozi wake kushindwa kuisimamia serikali katika kutekeleza miradi ya maendeleo.

Aidha amepongeza serikali ya awamu ya nne kwa namna ambavyo imedhamiria kwa dhati na kwa vitendo katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Kigoma jambo ambalo limerudisha imani ya wananchi kwa serikali na chama tawala.

Naye Rajabu Mwilima alisema kuwa uongozi wa sasa wa CCM unapaswa kusimamia maadili yake kikweli kweli hasa suala la vitendo vya rushwa katika chaguzi kwani vimekuwa vikishusha taswira nzuri ya chama hicho mbele ya jamii.

Mwilima alisema kuwa ana imani uongozi wa CCM ambao Makamu Mwenyekiti Philip Mangula ameingia utasaidia katika kurudisha taswira ya CCM kwenye kusimamia maadili ya uongozi, kanuni na uendeshaji wa chama ambao unajali maslahi ya jamii.

mwisho
 

BARAZA LA MADIWANI KUMC





Mkurugenzi wa manispaa ya Kigoma Ujiji Alfred Luanda akizungumza katika baraza la madiwani la manispaa hiyo (kushoto) Meya wa manispaa Ujiji, Bakari Beji.


Na Fadhili Abdallah,Kigoma

 BARAZA la madiwani la Halmashauri ya manispaa ya Kigoma Ujiji imeliomba jeshi la polisi nchini na mamlaka ya usalama wa usafiri wan chi kavu na majini (SUMATRA) waruhusu mabasi ya daladala katika manispaa hiyo kusimamisha abiria.

Wakizungumza wakati wa kikao cha kawaida cha baraza hilo baadhi ya madiwani ambao waliungwa mkono na Mkurugenzi wa manispaa ya Kigoma Ujiji, Alfred Luanda wamesimamia hoja yao hiyo inakuja kutokana na ukweli kwamba kumekuwa na tatizo kubwa kwa askari wa usalama barabarani katika kushughulikia jambo hilo.

Akitoa hoja kuhusiana na hilo Diwani wa kata ya Katubuka, Moses Bilantanye alisema kuwa askari wa usalama barabarani wamekuwa wakiwakamata na kuwatoza faini wenye daladala kwa kusimamisha abiria ambapo alihoji kuwa kwa nini likatazwe kigoma na mikoa mingine iruhusiwe kusimamisha abiria.

Bilantanye alisema kuwa kitendo cha askari barabarani kuzuia daladala kutosimamisha abiria kunaleta taabu kwa wanafunzi na kuwafanya wachelewe shule lakini pia huwafanya watu wanaosafiri na magari hayo kutumia muda mrefu vituoni kutokana na kukatiliwa kupanda kwenye magari hayo kwa vile abiria wameenea kwenye viti.

Akiunga mkono jambo Hilo, Naibu Meya wa manispaa ya Kigoma Ujiji, Yunus Ruhonvya na mkurugenzi wake, Alfred Luanda wamezitaka mamlaka hizo kutengua sheria hiyo kwa manispaa ya Kigoma Ujiji kama ambavyo kwa kutumia busara zao wameweza kutengua sheria hiyo kwa jiji la Dar es salaam.

Akijibu kuhusiana na hilo,Mkuu wa usalama wa barabarani mkoa Kigoma,Michael Stephen alisema kuwa kwa mujibu wa sheria ya usalama barabara ya mwaka 1973 kifungu cha 39(a) ni marufuku kwa gari la abiria kubeba mzigo  kuzidi  uzito ulioandikishwa wakati gari hilo linayengenezwa.

Alisema kuwa hapa nchini kumekuwa na tabia ya wamiliki wa magari ya daladala kuzifanyia marekebisho gari zao kwa kuweka viti ambavyo vimefanya magari hayo kubeba abiria zaidi ya uzito ambao gari husika limeandikishwa lakini kwa busara mamlaka husika vimekuwa vikiacha jambo hilo likiendelea na kusimamia katika kuhakikisha abiria zaidi hawasimamishwi.

Hata hivyo alisema kuwa ni mchakato mrefu kuruhusu magari ya abiria kubeba abiria zaidi ya uzito wake kwani uzito ambao gari inapaswa kuchukua inazingatia suala la usalama wa gari na abiria waliokuwemo na kwamba ofisi yake haiwezi kuruhusu jambo hilo bila kuzingatia suala la uslama wa gari linapokuwa kwenye mwendo.

Naye afisa wa SUMATRA mkoa kigoma, Adam Mamilo alisema kuwa amelichukua ombi hilo na ataliwasilisha kwa viongozi wake ambao baada ya kulitafakari na kuwa na vikao na wadau mbalimbali ndipo jibu la nini kifanyike linaweza kutolewa.

Mwisho.

VIJANA WANAOMALIZA MAFUNZO YA JKT WAKIPIGA RIGWARIDE

Vijana wanaomaliza mafunzo ya jeshi la kujenga taifa katika kambi ya JKT Burombola wilaya ya Kigoma mkoani Kigoma wakipita kwa mwendo wa kasi wakati wakitoa heshima kwa mgeni rasmiu

VIJANA WANAOMALIZA MAFUNZO YA JKT WAKIPIGA RIGWARIDE

Vijana wanaomaliza mafunzo ya jeshi la kujenga taifa katika kambi ya JKT Burombola wilaya ya Kigoma mkoani Kigoma wakipita kwa mwendo wa kasi wakati wakitoa heshima kwa mgeni rasmiu

DC AKIKAGUA MAZOEZI YA VIJANA JKT

 Mkuu wa wilaya Kigoma Ramadhani  Maneno (mwenye suti wa tatu kutoka kushoto) akiangalia mazoezi ya kupita kwenye eneo lenye vikwazo yaliyokuwa yakifanywa na vijana waliokuwa wakimaliz mafunzo ya kujitolea kambi ya JKT Burombola wilaya ya Kigoma Mkoani Kigoma



JESHI la kujenga taifa kikosi cha 821 Burombola mkoani Kigoma imesema kuwa haitaweza kufikia malengo ya uzalishaji waliyowekewa na makao makuu ya jeshi kutokana na kukabiliwa na mtaji mdogo na uharibifu wa wadudu waharibifu.

Akizungumza katika mahojiano maalum na gazeti hili Mkuu wa kambi hiyo, Meja Valentine Mrosso alisema kuwa kambi yake haitaweza kufikia uzalishaji wa hekari 600 walizopewa kutokana na changamoto hizo.

Alisema kuwa tatizo la mtaji kifedha, uharibifu unaofanywa na mchwa katika shamba la mahindi umechangia kurudisha nyuma malengo yao ya uzalishaji na kwamba kwa mwaka huu kambi hiyo imeweza kulima hekari 350 pekee.

Aidha Meja Mrosso alisema kuwa kambi yake haipati pembejeo za ruzuku ambazo zinatolewa kwa wakulima vijijini na serikali ambapo wameiomba serikali kuwaingiza katika utaratibu wa kupata pembejeo za ruzuku jambo ambalo litachangia kuwafanya waongeze uzalishaji.

Kwa upande wake meneja kilimo wa kambi hiyo, Adam Minzi alisema kuwa pamoja na changamoto hizo zinazowakabili lakini wamejiwekea malengo ya kuhakikisha wanalima hadi kufikia hekari 1000 katika kipindi cha miaka miwili ijayo.

Minzi alisema kuwa tayari wameshatoa taarifa kwa idara ya kilimo ya halmashauri ya wilaya kigoma kuhusiana na tatizo la mchwa ambao wamekuwa wakishambulia mahindi yaliyoanza kukomaa na hivyo kurudisha nyuma malengo ya uzalishaji.

Akizungumzia tatizo hilo Mkuu wa wilaya kigoma, Ramadhani Maneno alisema kuwa pamoja na malengo yaliyowekwa ya kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo lakini pia kambi za JKT na magereza mkoani humo ni maeneo ambayo mkoa unatarajia yatachangia kuongeza uzalishaji katika utekelezaji wa mkakati wa kilimo kwanza.

Maneno alisema kuwa tayari ameshatoa maelekezo kwa idara ya kilimo ya halmashauri ya wilaya kigoma kulifanyia kazi tatizo la mchwa linaloikabili kambi hiyo ya Burombola ili kuweza kukabiliana na athari ambazo zitaweza kutokea.

Mwisho.