Waziri wa uchukuzi Harison Mwakyembe (wa pili kushoto) akitunuku cheti
kwa amina Hussein (kulia) mmoja wa wahitimu 28 wa Diploma ya hali ya
hewa wakati wa mahafali ya chuo cha hali ya hewa mjini Kigoma kwa mwaka huu 2012
(picha na Fadhili Abdallah)
Waziri wa
uchukuzi Harison Mwakyembe ameiagiza mamlaka ya hali ya hewa nchini( TMA)
kufanya utafiti na kuon namna gani wanaweza kuwasaidia wananchi kukabiliana
radi zinazotokea na kuwadhulu watu wengi nchini kila siku.
Akizungumza
katika mahafali ya kuwatunuku vyeti wahitimu wa mafunzo ya diploma ya hali ya
hewa katika chuo cha hali ya hewa kigoma Mwakyembe alisema kuwa n lazima
wahitimu waonyeshe umahiri wao katika kuwasaidia wananchi kutokana na taaluma
wanayopata.
Aalisema kuwa
idara ya hali ya hewa imekuwa na umuhimu mkubwa kwa maisha ya wananchi lakini
umuhimu huo usiishie kwenye utabiri tu lazima wasomi wanaohitimu mafunzo katika
vyuo vya hali ya hewa ndani na nje ya nchi kuwasaidia wananchi kuona namna gani
tenkolojia ya kukabiliana na radi inaweza kuwasaidia wananchi.
Aidha sambamba
na hilo waziri huyo wa uchukuzi alisema kuwa mamlaka haina budi kurahisisha
utabiri wa hali ya hewa na kuufanya uwe na manufaa ya moja kwa moja kwa
mwananchi ili jamii na taifa liweze kupanga mipango yake kwa kuzingatia utabiri
unaotolewa na idara hiyo.
Waziri Mwakyembe
alisema kuwa ili kwenda na wakati na wananchi waone umuhimu wa uwepo wa taasisi
hiyo ni budi TMA ianze kutoa utabiri wa hali ya hewa kwa maeneo
madogo pamoja na elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa utabiri wa hali ya hewa.
kwa upande wake
mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya hali ya hewa nchini,Dk.A gnes kijazi amesema
katika kuboresha shughuli za mamlaka , wako katika hatua za mwisho kwa
kushirikiana na chuo kikuu cha Dar es salaam kuanza kutoa shahada ya hali ya
hewa.
Dk.Kijazi
alisema kuwa hata hivyo ufinyu wa bajeti umekuwa ukikwaza utekelezaji wa
mipango mbalimbali ya kimaendeleo ya mamlka hiyo na kwamba kwa mwaka ujao
serikali imeahidi kuiongeza bajeti mamlaka hiyo ili iweze kutekeleza mipango
yake kwa manufaa ya nchi.
kwa upande wao
wahitimu wa mafunzo hayo , pamoja na kuelezea matumaini yao baada ya kumaliza
masomo , wameiomba serikali kuyapatia ufumbuzi matatizo ya maabara, vitabu,
majengo na usafiri yanayokikabili chuo hicho pekee cha hali ya hewa nchini.
Mmoja wa
wahitimu hao, Shaban Dilunga akisoma
risala kwa niaba ya wajitimu hao alisema kuwa pamoja na changamoto hizo lakini
ufinyu wa bajeti na uchache wa fedha wanazipowa umechangia kuwafanya washindwe
kufanya mafunzo kwa vitendo (Field na study tour).
mwisho
No comments:
Post a Comment