MKUU wa mkoa Kigoma Issa Machibya amewataka wahitimu wa kozi
ya mgambo kuzingatia nidhamu na kutumia mafunzo hayo kwa ajili ya kusaidia
shughuli mbalimbali za kijamii badala ya kuwa chanzo cha kuwaingiza kwenye
vitendo vya kihalifu.
Machibya alisema hayo katika hotuba iliyotolewa kwa niaba
yake na Mkuu wa wilaya Kigoma, Ramadhani Maneno wakati wa kufunga mafunzo ya
mgambo kwa watumishi 168 wa serikali mkoani Kigoma yaliyoenda sambamba na
maadhimisho ya miaka 51 ya uhuru.
Mkuu huyo wa mkoa amesema kuwa serikali ya mkoa imeamua
kufanyika kwa mafunzo hayo lengo likiwa kuwajengea ukakamavu watumishi wake
lakini pia kuongeza uzalendo miongoni mwa watumishi wake hasa vijan ambao
wameanza kazi miaka ya hivi karibuni.
Awali katika risala ya wahitimu hao iliyosomwa kwa niaba yao
na Noel Byamungu wamesema kuwa kumekuwa wamekuwambana na changamoto mbalimbali katika
mafunzo hayo ikiwemo kitendo cha mwajiri kushindwa kuwalipa stahili zao kwa
wakati.
Byamungu alisema kuwa kitendo kimechangia kuwafanya washiriki kutoshiriki mafunzo kwa
uhuru lakini kwani kimekuwa kikiharibu bajeti zao ambapo wameahidi kwamba
watatumia mafunzo hayo kwa kadri ya kiapo walichokula kwa maslahi ya Watanzania
wote.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment