Na Mwandishi Wetu,Kasulu
Rais Jakaya Kikwete amesema kuwa serikali haitawavumilia waumin wachache
wa madhehebu ya dini wanaotaka kuvuruga amani ya nchi kwa maslahi yao
na kwamba hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa wote watakaobainika
kuhusika katika kuchochea vurugu za kidini zinazoendelea nchini.
Raisi Kikwete alitoa kauli hiyo wilayani Kasulu mkoani Kigoma katika
hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na waziri wa mambo ya nje na
ushirikiano wa kimataifa Bernad Membe wakati wa harambee ya kuchangisha
fedha za ujenzi wa kanisa katoliki la mtakatifu petro mtume kigango cha
Murubona wilayani kasulu.
kwa upande wake kiongozi wa kanisa hilo , padre Castus Rwegoshora
amesema kuwa zaidi ya shilingi milioni mia mbili zinahitajika ili
kukamilisha ujenzi wa kanisa hilo litakalokuwa na uwezo wa kuchukua
waumin elfu mbili kwa wakati mmoja.
Katika harambee hiyo zaidi ya shilingi milioni sabini zilipatikana
huku huyo wa mambo ya nchi za nje na rafiki zake wakichangia shilingi
milioni hamsini.
mwisho
No comments:
Post a Comment