Na Fadhili
Abdallah,Kigoma
POLISI mkoani Kigoma imempiga risasi na kumuua mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Lowasi Moria anayesadikiwa kuwa jambazi aliyekuwa kwenye mkakati wa kufanya uporaji wa kutumia bunduki kwa mfanyabiashara mmoja wilayani humo.
Kamanda wa Polisi mkoa Kigoma, Fraiser Kashai alisema mjini hapa kwamba kabla ya kutokea mauaji hayo kulitokea kutupiana risasi kati ya polisi na majambazi hayo yaliyokuwa manne na ndipo jambazi mmoja aliuawa na wengine watatu kukimbia.
Kamanda Kashai alisema kuwa baada ya mpambano huo wa kutupiana risasi kati ya polisi na majambazi bunduki moja aina ya SMG iliyokuwa na risasi nne kwenye magazine iliyokuwa ikitumiwa na majambazi hayo imekamatwa.
Akieleza kuhusu tukio hilo Kamanda huyo wa polisi mkoa kigoma alisema kuwa awali polisi ilipata taarifa kutoka kwa raia wema kuhusu uwepo wa watu wanne waliokuwa na bunduki ambao walikuwa kwenye mpango wa kumvamia mfanyabiashara mmoja aliyekuwa anasafiri na pikipiki kutoka kakonko kwenda Muhange akiwa na fedha kiasi cha shilingi milioni 12.
Alisema kuwa kufuatia taarifa hizo ;polisi waliweka mtego mahali panapoelezwa kutaka kutokea tukio hilo na ndipo kabla mfanyabiashara huyo hajapita eneo hilo polisi waliwavamia majambazi hayo na kuanza kurushiana risasi zilizopelekea kifo cha jambazi mmoja na wengine watatu kukimbia.
Katika tukio lingine polisi mkoani Kigoma inamshikilia Sara Dasse mkazi wa kijiji cha Mpeta tarafa ya Nguruka mkoani Kigoma kwa tuhuma za kumkaba na kumuua mtoto wake wa kumzaa aitwaye Zainabu Sitta mwenye umri wa mwaka mmoja.
Kamanda wa polisi mkoani Kigoma, Fraiser Kashai alisema kuwa polisi inaendelea na uchunguzi kuhusiana na mazingira yaliyosababisha kifo hicho lakini alisema kuwa habari za kuaminika zinaeleza kuwa mtuhumiwa anasumbuliwa na maradhi ya akili kwa maana ya ukichaa.
mwisho.

No comments:
Post a Comment