Saturday, June 9, 2012



Na Fadhili Abdallah,Kigoma

Mwanadada Anna Wilbroad juzi usiku alifanikiwa kunaykua  taji la mnyange wa mkoa Kigoma kwa mwaka 2012 baada ya kuwashinda washiriki wenzake saba walishiriki kinyang'anyiro hicho kwa mwaka huu.


Akitangaza matokeo ya ushindi Jaji mkuu wa mashindano hayo Rashidi Michumino kutoka ofisi ya mkurugenzi wa manispaa ya kigoma Ujiji alisema kuwa pamoja na kunyakua taji hilo mnyange huyo pia atapata zawadi ya fedha taslim kiasi cha shilingi 300,000 na kushiriki katika mashindano ya kanda mkoani Dodoma.

Pamoja na zawadi hizo pia mshindi huyo amepata zawadi ya kusoma kozi ya masomo ua utalii kwa mwaka mmoja katika chuo cha western Tanganyika cha mjini kigoma huku.

Mshindi wa pili katika shindano hilo ulinyakuliwa na mrembo Susan Gregory aliyepata zawadi ya shilingi 200,000 kozi ya masomo ya utalii kwa mwaka mmoja akipata nafasi pia ya kushiriki mashindano ya ngazi ya kanda mkoani Dodoma.

Jaji wa shindano alimtangaza mwanadada Justina Philipo kuwa mshindi wa tatu ambaye alipata zawadi ya fedha taslim kiasi cha shilingi 100,000 kozi ya miezi ya Computer akipata nafasi pia ya kushiriki katika mashindano ngazi ya kanda.

Mwanadada Mwamvita Juma aliibuka kuwa mshindi katika shindano la vipaji na ubunifu ambapo alizawadiwa kiasi cha shilingi 50,000 katika shindano ambalo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya kigoma, Lilian Mbaga alikuwa mgeni rasmi.

Akikabidhi zawadi kwa washindi Mkurugenzi huyo wa Halmashauri ya wilaya kigoma alitoa wito kwa wazazi kuwaruhusu watoto wao kushiriki shindano hilo ambalo kwa sasa limekuwa pia chanzo cha ajira kwa wasichana wanaofanya vizuri na wenye vipaji.

mwisho.

No comments:

Post a Comment