Thursday, June 14, 2012

KAMANDA WA POLISI KIGOMA FRAISSER KASHAI

KAMANDA WA POLISI MKOA KIGOMA FRAISSER KASHAI AKITOA TAARIFA MBALIMBALI KWA WAANDISHI WA HABARI

ADAKWA NA RISASI KIBAO

MAMIA YA RISASI KAMA YANAVYOONEKANA AMBAYO POLISI WALIMDAKA MTU MMOJA ANAYETUHUMIWA KUWA NI JAMBAZI KATIKA MPAKA WA TANZANIA NA BURUNDI

Tuesday, June 12, 2012

JKT KANEMBWA MABINGWA WA SOKA KIGOMA


Na Fadhili Abdallah,Kigoma

TIMU ya soka ya JKT Kanembwa ya wilaya ya kibondo mkoani Kigoma imefanikiwa kunyakua ushindi wa kwanza wa mashindano ya ligi ya taifa ngazi ya Taifa Kituo cha Kigoma baada ya kuibuka na pointi 16 ambazo hazikuweza kufikiwa na timu nyingine sita zilizoshiriki mashindano hayo.

katika mashindano hayo mabingwa hao waliweza kushinda michezo yao mitano na kutoka sare mchezo mmoja na hivyo ushindi huo unaipa tiketi timu hiyo ya Kigoma kucheza ligi daraja la kwanza nchini.

Ushindi wa pili katika kituo hicho cha Kigoma ulichukuliwa na timu ya mwadui ya shinyanga ambayo imeweza kufikisha point 11 baada ya kushinda michezo yake mitatu kutoa sare michezo miwili ambapo ilipoteza mchezo mmoja.


kufuatia kushika nafasi ya pili timu hiyo ya mwadui kutoka shinyanga italazimika kucheza ligi ndogo itakayojumuisha washindi wa pili kutoka vituo vingine ili kupata timu mbili zitakazoungana na timu zilizofuzu kwa ajili ya mshindano ya ligi daraja la kwanza.

Akizungumzia matokeo hayo Kocha wa timu ya JKT Kanembwa Saidi Mdoe amesema kuwa watalazimika kufanya usajili ili kupata wachezaji wa kukiongezea nguvu kikosi chake ili kifanye vizuri kuiwezesha timu hiyo kucheza ligi kuu nchini baada ya miaka 20 ya mkoa Kigoma kupotea katika mashindano hayo.


Kwa upande wake Katibu wa chama cha soka mkoa Kigoma Mrisho Bukuku amesema kuwa  timu hiyo inahitaji kupata wachezaji wenye uwezo wa kuhimili mikiki mikiki ya ligi hiyo daraja la kwanza na kuweza kuipandisha timu hiyo katika ligi kuu nchini.

katika kuunga mkono mafanikio ya timu hiyo Bukuku amesema kuwa uongozi wa serikali wilaya ya kibondo kwa kushirikiana na Mkuu wa mkoa Kigoma, Issa Machibya wamejipanga kutafuta fedha za kuiwezesha timu hiyo kufanya maandalizi ya kutosha na kupata mafanikio katika michezo yake.

mwisho

POLISI YAUA JAMBAZI KIGOMA


Na Fadhili Abdallah,Kigoma

POLISI mkoani Kigoma imempiga risasi na kumuua mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Lowasi Moria anayesadikiwa kuwa jambazi aliyekuwa kwenye mkakati wa kufanya uporaji wa kutumia bunduki kwa mfanyabiashara mmoja wilayani humo.

Kamanda wa Polisi mkoa Kigoma, Fraiser Kashai alisema mjini hapa kwamba kabla ya kutokea mauaji hayo kulitokea kutupiana risasi kati ya polisi na majambazi hayo yaliyokuwa manne na ndipo jambazi mmoja aliuawa na wengine watatu kukimbia.

Kamanda Kashai alisema kuwa baada ya mpambano huo wa kutupiana risasi kati ya polisi na majambazi bunduki moja aina ya SMG iliyokuwa na risasi nne kwenye magazine iliyokuwa ikitumiwa na majambazi hayo imekamatwa.

Akieleza kuhusu tukio hilo Kamanda huyo wa polisi mkoa kigoma alisema kuwa awali polisi ilipata taarifa kutoka kwa raia wema kuhusu uwepo wa watu wanne waliokuwa na bunduki ambao walikuwa kwenye mpango wa kumvamia mfanyabiashara mmoja aliyekuwa anasafiri na pikipiki kutoka kakonko kwenda Muhange akiwa na fedha kiasi cha shilingi milioni 12.

Alisema kuwa kufuatia taarifa hizo ;polisi waliweka mtego mahali panapoelezwa kutaka kutokea tukio hilo na ndipo kabla mfanyabiashara huyo hajapita eneo hilo polisi waliwavamia majambazi hayo na kuanza kurushiana risasi zilizopelekea kifo cha jambazi mmoja na wengine watatu kukimbia.


Katika tukio lingine polisi mkoani Kigoma inamshikilia Sara Dasse mkazi wa kijiji cha Mpeta tarafa ya Nguruka mkoani Kigoma kwa tuhuma za kumkaba na kumuua mtoto wake  wa kumzaa aitwaye Zainabu Sitta mwenye umri wa mwaka mmoja.

Kamanda wa polisi mkoani Kigoma, Fraiser Kashai alisema kuwa polisi inaendelea na uchunguzi kuhusiana na mazingira yaliyosababisha kifo hicho lakini alisema kuwa habari za kuaminika zinaeleza kuwa mtuhumiwa anasumbuliwa na maradhi ya akili kwa maana ya ukichaa.

mwisho.

Saturday, June 9, 2012

WAREMBO KABLA YA KUJUA HATIMA YAO WAKAANZA HIVI NA MGONGO KUUMA
WADAU PIA HAWAKUKOSA KILA MMOJA ALIHANGAIKA KIVYAKE KUTAFUTA PICHA NZURI KWA AJILI YA UKUMBUSHO WA TUKIO HILO


Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya Kigoma,Lilian Mbaga ( wa kwanza Kulia) akiwa na warembo wa mkoa Kigoma kwa mwaka huu wa 2012, aliyekaa ni mshindi wa kwanza Anna Willbroad, Mshindi wa pili Suzan Gregory (wa pili kulia) na mshindi wa tatu, Justina Philipo (kushoto)
warembo wa mkoa Kigoma kwa mwaka huu wa 2012, aliyekaa ni mshindi wa kwanza Anna Willbroad, Mshindi wa pili Suzan Gregory (wa pili kulia) na mshindi wa tatu, Justina Philipo (kushoto)

(Picha na Fadhili Abdallah)

Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya Kigoma,Lilian Mbaga ( wa kwanza Kulia) akiwa na warembo wa mkoa Kigoma kwa mwaka huu wa 2012, aliyekaa ni mshindi wa kwanza Anna Willbroad, Mshindi wa pili Suzan Gregory (wa pili kulia) na mshindi wa tatu, Justina Philipo (kushoto)

(Picha na Fadhili Abdallah)




Na Fadhili Abdallah,Kigoma

Mwanadada Anna Wilbroad juzi usiku alifanikiwa kunaykua  taji la mnyange wa mkoa Kigoma kwa mwaka 2012 baada ya kuwashinda washiriki wenzake saba walishiriki kinyang'anyiro hicho kwa mwaka huu.


Akitangaza matokeo ya ushindi Jaji mkuu wa mashindano hayo Rashidi Michumino kutoka ofisi ya mkurugenzi wa manispaa ya kigoma Ujiji alisema kuwa pamoja na kunyakua taji hilo mnyange huyo pia atapata zawadi ya fedha taslim kiasi cha shilingi 300,000 na kushiriki katika mashindano ya kanda mkoani Dodoma.

Pamoja na zawadi hizo pia mshindi huyo amepata zawadi ya kusoma kozi ya masomo ua utalii kwa mwaka mmoja katika chuo cha western Tanganyika cha mjini kigoma huku.

Mshindi wa pili katika shindano hilo ulinyakuliwa na mrembo Susan Gregory aliyepata zawadi ya shilingi 200,000 kozi ya masomo ya utalii kwa mwaka mmoja akipata nafasi pia ya kushiriki mashindano ya ngazi ya kanda mkoani Dodoma.

Jaji wa shindano alimtangaza mwanadada Justina Philipo kuwa mshindi wa tatu ambaye alipata zawadi ya fedha taslim kiasi cha shilingi 100,000 kozi ya miezi ya Computer akipata nafasi pia ya kushiriki katika mashindano ngazi ya kanda.

Mwanadada Mwamvita Juma aliibuka kuwa mshindi katika shindano la vipaji na ubunifu ambapo alizawadiwa kiasi cha shilingi 50,000 katika shindano ambalo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya kigoma, Lilian Mbaga alikuwa mgeni rasmi.

Akikabidhi zawadi kwa washindi Mkurugenzi huyo wa Halmashauri ya wilaya kigoma alitoa wito kwa wazazi kuwaruhusu watoto wao kushiriki shindano hilo ambalo kwa sasa limekuwa pia chanzo cha ajira kwa wasichana wanaofanya vizuri na wenye vipaji.

mwisho.

1.PICHA YA JUU NI WAANDISHI WA HABARI WA MKOA KIGOMA WAKIONGOZWA NA MWENYEKITI WAO DEO NSOKOLO KATIKATI WAKITAFAKARI MAMBO KATIKA HOTEL YA LAKE TANGANYIKA MJINI KIGOMA.



2.MKUU WA WILAYA KIGOMA RAMADHANI MANENO AKIFUNGUA MKUTANO WA WADAU WA MAZINGIRA ULIO CHINI YA MRADI WA MAENDELEO YA BONDE LA ZIWA TANGANYIKA

3.MENEJA WA MRADI WA MAENDFELEO YA BONDE LA ZIWA TANGANYIKA HAWA MSHAMU AKIZUNGUMZA KATIKA MKUTANO WA WATAALAM NA WADAU WA MAZINGIRA KUTOKA WILAYA TATU ZA MKOA KIGOMA NA ZA MKOA KATAVI KUHUSU KUELEZEA HATUA MBALIMBALI ZA UHIFADHI NA UTUNZAJI WA MAZINGIRA YA BONDE LA ZIWA TANGANYIKA (PICHA NA FADHILI ABDALLAH)

USIMAMIZI WA SHERIA KIKWAZO UTUNZAJI MAZINGIRA


Na Fadhili Abdallah,Kigoma

USIMAMIZI wa sheria za utunzaji na uhifadhi mazingira umekuwa ni changamoto kubwa katika kuufanya mradi wa maendeleo ya bonde la ziwa Tanganyika kupata mafanikio kwani kwa hali ya sasa mradi hauwezi kuchukua hatua kuhusiana na watu wanaoharibu mazingira.

Meneja wa Mradi huo, Hawa Mshamu alisema hayo katika ziara ya kutembelea baadhi ya maeneo ya utekelezaji wa mradi ziara inayotokana na mkutano wa siku moja wa wadau kupeana taarifa ya hali ya maendeleo ya mradi huo.

Alikuwa akijibu baadhi ya maswali ya wajumbe wa ziara hiyo waliotaka kujua uongozi wa mradi unachukua hatua gani kwa watu wanaokaidi kutekeleza vipengele vya utekelezaji wa mradi au wanaohareibu mazingira.

Mshamu alisema kuwa kazi kubwa ya mradi ni kutoa elimu kwa jamii ya nini kifanyike kwa manufaa ya siku za baadaye pamoja na kuendesha miradi mbalimbali ya utunzaji na uhifadhi mazingira ikiwemo upandaji miti na miradi ya kujiingizia kipato kwa jamii katika baadhi ya vijiji vya mradi huo.

Akizungumza katika mkutano huo wa siku moja mkurugenzi wa mazingira wa  mamlaka ya bonde la ziwa Tanganyika (LTA) Gabriel Hakizimana alisema kuwa yapo mafanikio ambayo yameptaikana tangu kuanza kwa mradi ingawa zipo changamoto ambazo bado zinatakiwa kufanyiwa kazi zaidi.

Hakizimana alisema kuwa kikubwa zaidi elimu na uhamasishaji jamii unatakiwa kufanywa kwa nguvu kubwa ili kuifanya jamii itambue umuhimu wa utunzaji na uhifadhi wa bonde la ziwa Tanganyika kwa kipindi kirefu kijacho na kwamba vyombo vya habari vinayo kazi kubwa katika kushiriki katika mkakati huo.

Mkurugenzi huyo alisema kuwa ziwa Tanganyika ni urithi wa dunia likiwa na zaidi ya aina 600 za viumbe ambapo kati yake 200 havipatikani mahali popote zaidi ya ndani ya ziwa hilo na kwamba  upo umuhimu mkubwa kwa jamii inayozunguka ziwa hilo na nchi ambazo ziwa hilo lipo kulitunza kwa hali na mali.

Akifungua mkutano huo Mkuu wilaya kigoma, Ramadhani Maneno alisema kuwa wananchi wanapaswa kulifanya suala la uhifadhi na utunzaji mazingira ya bonde la ziwa Tanganyika kuwa sehemu ya maisha yao kutokana na umuhimu wa ziwa hilo.

Maneno alisema kuwa pamoja na ufadhili wa wahisani wa nje lakini pia serikali itaweka mkakati wa kuhakikisha fedha za utunzaji na uhifadhi wa mazingira katika halmashauri zinapatikana sambamba na kuzisimamia kwa karibu sheria za utunzaji na uhifadhi huo wa mazingira.

Mwisho.