Friday, July 18, 2014


VIONGOZI WA CHADEMA MKOA WANG’ATUKA.
“Kuanzia leo tarehe 18/07/2014, sisi si wanachama wala viongozi wa  CHADEMA tena”. Kauli hii imetolewa  na mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo wa mkoa wa Kigoma wakati akiongea na waandishi wa habari.
 Mwanyekiti huyo Bwana Jafari Ramdhani Kasisiko, aliyekuwa ameongozana na Katibu wa mkoa wa chama cha demokrasia na maendeleo, bwana Msafiri Wamarwa, pamoja  na katibu wa baraza la wanawake Chadema bi. Malunga Masudi  Simba wametangaza kujitoa rasmi kutokana na sababu mbalimbali.
Akiziongea sababu hizo bwana Kasisiko alisema kuwa chama cha CHADEMA kimepoteza sifa ya demokrasia na kuwa chama cha kibabe ambacho kinaongozwa na watu wachache, jambo ambalo yeye hayupo tayari kuungana nalo mkono.
Akitoa mfano, Kasisiko alisema kuwa “ hakuna  sheria, kanuni, wala taratibu  katika chama inayomkataza mwanachama kugombea nafasi za uongozi kitaifa, lakini alipotaka kugombea ukatibu wa taifa, bwana Zitto Kabwe, yaliibuka mambo mengi yaliyomfanya mpaka sasa ashikiriwe na mahakama”

 (Katikati ni Menyeketi wa CHADEMA mkoa wa Kigoma bwana Jafari Kasisiko, kushoto kwake ni katibu wa BAWACHA bi. Malunga Simba, na kulia kwake ni katibu wa CHADEMA mkoa bwana Mafiri Wamarwa)

Kwa upande wake bwana Wamarwa, amesema kuwa, wameamua kujitoa si kwa kumfuata mtu yeyote, bali wamekaa na kulitafakari jambo hili kwa muda mrefu, na hivyo maamuzi waliyofikia ni ya kwao kwaajili ya maslahi ya demokrasia.
Naye bi. Masudi alisema kuwa, wamejitoa kwa mapenzi, nia na moyo wao kwani wameona hakina faida na wananchi  kwakuwa kimekiuka utaratibu wa kuwatetaea na kuwapigania wananchi walio wengi na kufuata misingi ya watu wachache.
Zaidi ya hayo mwenyekiti huyo alisema kuwa, hawakujitoa ili kuwavunja moyo wanachama wengine wa CHADEMA kwani chama hicho ni kikubwa, kina mtazamo mzuri wa kuingoza nchi na wapo viongozi wengine watakaochukua gurdumu hilo la uongozi na kukifanya chama hicho kizidi kushamiri.


Thursday, July 3, 2014




USAFI WA KALAKANA KWAAJILI YA UUNDAJI WA MELI  MBIONI KUKAMILIKA.

Imekuwa ni kipindi kirefu tangu  mwaka 1965 ambapo kalakana ya mkoa wa Kigoma ilipofanyiwa usafi kwa mara ya mwisho, kalakana hiyo sasa inafanyiwa usafi kwa mara nyingine ikiwa katika maandalizi ya uundaji wa meli.

Akiongea na vyombo vya habari mkoani humo, Kaimu  Mkuu wa bandari ya Kigoma bw. David Katembo  amesema kumekuwa na kazi nzito ya kutoa maji na tope katika kalakana hiyo ambayo sasa ipo katika hatua nzuri nakwamba ifikapo mwezi septemba mwaka huu usafi huu utakuwa umekamlilka.

Amesema kuwa zaidi ya viroba 20,000 vya mchanga vimewekwa mita sita kwenda aridhini katika eneo la mlango wa maji ili kuziba maji hayo yasiingie katika eneo la kalakana.

Kwa upande wake injinia wa mrdi bw. Yoeza Senzighe  amesema kuwa lengo lakufanya usafi katika kalakana ni kuhakikisha kuwa vyuma, minyororo, nati pamoja na reli vinakuwa safi ili kujua kipi kimeharibika kwaajili ya matengenezo zaidi kabla uundaji wa meli haujaanza.


Amesema lengo kuu la kuiandaa kalakana hiyo ni uundaji wa meli mpya pamoja na matengenezo mengine ya meli pale zinapokuwa zimeharibika.

Zaidi  bwana Senzighe amezieleza baadhi ya changamoto zinazowakabili katika ukarabati wa kalakana hiyo ikiwa ni pamoja na maji ya asili yaliyopo katika eneo hlio ambayo yanasababisha malngo wa maji usiweze kuzibika moja kwa moja.

Mwisho.  



Thursday, June 26, 2014




Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA,Witness Shoo amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kutoka klabu ya waandishi wa habari wa Kigoma wanaofanya ziara ya mafunzo kutembelea hifadhi mbalimbali nchini.

Shoo alisema kuwa kuendelea kuuawa kwa tembo na faru kunatishia kutoweka kwa wanyama hao ambao wamekuwa na mchango mkubwa katika sekta ya utalii kutokana na idadi kubwa ya watalii wanaotembelea hifadhi mbalimbali nchini kuwa na shauku ya kuwaona wanyama hao.

Katika kukabiliana na changamoto hiyo Mkurugenzi huyo wa TANAPA amewaomba waandishi wa habari kutumia vyombo vyao katika kufichua na kuandika bila woga kuhusiana na ujangiri na kuwatangaza majangiri wanaokamatwa.

Sambamba na kuandika na kufichua masuala ya ujangiri Shoo amewataka waandishi wa habari kuandika kwa wingi na kuhamasisha jamii ya Watanzania umuhimu wa kutembelea hifadhi zetu.

Kwa upande wake Afisa Habari wa TANAPA, Pascal Shelutete amesema kuwa waandishi wa habari wamekuwa na mchango mkubwa katika kukuza na kuendeleza sekta ya utalii hasa katika kuvitangaza vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo nchini.

Shelutete alisema kuwa mchango wa waandishi wa habari umekuwa na faida kubwa na umechangia kuongeza idadi ya Watanzania kama watalii wa ndani kutembelea hifadhi mbalimbali nchini.

Mwisho.



 

Mhifadhi Utalii katika hifadhi ya Taifa ya Arusha  Sakinoi mwenye jaketi akieleza namna nyati alivyouawa kwa mitego ya waya kunakofanywa na majangiri


Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA witness Shoo (kushoto) akizungumza na waandisha wa habari kutoka Kigoma Press Club waliokuwa wakifanya ziara ya utalii wa ndani kutembelea hifadhi mbalimbali nchini hapa ni makao makuu ya TANAPA mjini Arusha.

(Picha na Fadhili Abdallah)