USAFI WA KALAKANA KWAAJILI YA UUNDAJI WA MELI MBIONI KUKAMILIKA.
Imekuwa ni kipindi kirefu tangu mwaka 1965 ambapo kalakana ya mkoa wa Kigoma
ilipofanyiwa usafi kwa mara ya mwisho, kalakana hiyo sasa inafanyiwa usafi kwa
mara nyingine ikiwa katika maandalizi ya uundaji wa meli.
Akiongea na vyombo vya habari mkoani humo, Kaimu Mkuu wa bandari ya Kigoma bw. David Katembo amesema kumekuwa na kazi nzito ya kutoa maji
na tope katika kalakana hiyo ambayo sasa ipo katika hatua nzuri nakwamba
ifikapo mwezi septemba mwaka huu usafi huu utakuwa umekamlilka.
Amesema kuwa zaidi ya viroba 20,000 vya mchanga vimewekwa mita
sita kwenda aridhini katika eneo la mlango wa maji ili kuziba maji hayo
yasiingie katika eneo la kalakana.
Kwa upande wake injinia wa mrdi bw. Yoeza Senzighe amesema kuwa lengo lakufanya usafi katika
kalakana ni kuhakikisha kuwa vyuma, minyororo, nati pamoja na reli vinakuwa
safi ili kujua kipi kimeharibika kwaajili ya matengenezo zaidi kabla uundaji wa
meli haujaanza.
Amesema lengo kuu la kuiandaa kalakana hiyo ni uundaji wa
meli mpya pamoja na matengenezo mengine ya meli pale zinapokuwa zimeharibika.
Zaidi bwana Senzighe
amezieleza baadhi ya changamoto zinazowakabili katika ukarabati wa kalakana
hiyo ikiwa ni pamoja na maji ya asili yaliyopo katika eneo hlio ambayo
yanasababisha malngo wa maji usiweze kuzibika moja kwa moja.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment