VIONGOZI WA CHADEMA MKOA WANG’ATUKA.
“Kuanzia leo tarehe 18/07/2014, sisi si wanachama
wala viongozi wa CHADEMA tena”. Kauli hii
imetolewa na mwenyekiti wa chama cha demokrasia
na maendeleo wa mkoa wa Kigoma wakati akiongea na waandishi wa habari.
Mwanyekiti huyo Bwana Jafari Ramdhani Kasisiko, aliyekuwa
ameongozana na Katibu wa mkoa wa chama cha demokrasia na maendeleo, bwana Msafiri
Wamarwa, pamoja na katibu wa baraza la wanawake
Chadema bi. Malunga Masudi Simba
wametangaza kujitoa rasmi kutokana na sababu mbalimbali.
Akiziongea sababu hizo bwana Kasisiko alisema kuwa
chama cha CHADEMA kimepoteza sifa ya demokrasia na kuwa chama cha kibabe
ambacho kinaongozwa na watu wachache, jambo ambalo yeye hayupo tayari kuungana
nalo mkono.
Akitoa mfano, Kasisiko alisema kuwa “ hakuna sheria, kanuni, wala taratibu katika chama inayomkataza mwanachama kugombea
nafasi za uongozi kitaifa, lakini alipotaka kugombea ukatibu wa taifa, bwana
Zitto Kabwe, yaliibuka mambo mengi yaliyomfanya mpaka sasa ashikiriwe na
mahakama”
(Katikati ni Menyeketi wa CHADEMA mkoa wa Kigoma bwana Jafari Kasisiko, kushoto kwake ni katibu wa BAWACHA bi. Malunga Simba, na kulia kwake ni katibu wa CHADEMA mkoa bwana Mafiri Wamarwa)
Kwa upande wake bwana Wamarwa, amesema kuwa, wameamua
kujitoa si kwa kumfuata mtu yeyote, bali wamekaa na kulitafakari jambo hili kwa
muda mrefu, na hivyo maamuzi waliyofikia ni ya kwao kwaajili ya maslahi ya
demokrasia.
Naye bi. Masudi alisema kuwa, wamejitoa kwa mapenzi,
nia na moyo wao kwani wameona hakina faida na wananchi kwakuwa kimekiuka utaratibu wa kuwatetaea na
kuwapigania wananchi walio wengi na kufuata misingi ya watu wachache.
Zaidi ya hayo mwenyekiti huyo alisema kuwa,
hawakujitoa ili kuwavunja moyo wanachama wengine wa CHADEMA kwani chama hicho
ni kikubwa, kina mtazamo mzuri wa kuingoza nchi na wapo viongozi wengine
watakaochukua gurdumu hilo la uongozi na kukifanya chama hicho kizidi
kushamiri.
No comments:
Post a Comment