Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwapungia wananchi wa mkoa Kigoma waliofika kumpokea kwenye uwanja wa ndege wa Kigoma
Waziri Mkuu mizengo Pinda akipeana mkono na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene ambaye alikuwa miongoni mwa mawaziri walioshiriki ziara ya siku sita ya Waziri mkuu Mizengo Pinda mkoani Kigoma
waziri Mkuu Mizengo Pinda akisalimia na mbunge wa jimbo la Kasulu Vijijini Agripina Buyogera muda mfupi baada ya waziri Mkuu kuwasili uwanja wa ndege wa kigoma kwa ziara ya kiserikali ya siku sita mkoani humo.
Karibu Kigoma ndiyo anavyoelekea kusema Mkuu wa mkoa Kigoma Kanali Mstaafu, Issa Machibya (kushoto) akimkaribisha Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliyeanza ziara ya kiserikali ya siku sita mkoani Kigoma (Picha zote na Fadhili Abdallah)
Uzinduzi wa uvinza fm
ReplyDeleteUVINZA
Wakazi wa wilaya ya UVINZA na vijiji vya jirani mkoani KIGOMA wamenufaika na uzinduzi wa mradi wa UVINZA FM utakaotumika kuhamasisha, amani, demokrasia na maendeleo .
Mradi huo umezinduliwa hivi karibuni katika ukumbi wa vijana UVINZA ukiwa ni miongoni mwa Redio 26 zinazotekeleza barani afrika ikiwa ni mchakato wa demokrasia kupitia vyombo vya habari.
Mradi huo unaofadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni- UNESCO kwa kushirikiana na Shirika jingine la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo -UNDP.
Katika hotuba iliyosomwa na mkuu wa wilaya ya UVINZA Bi. HADIJA NYEMBO kwa niaba ya mkuu wa mkoa LUTENI KANALI MSTAAFU ISSA MACHIBYA amehimiza utendaji kazi kwa bidii na utekelezaji wa majukumu ya UVINZA FM ili kukuza na kudumisha mawasiliano yatakayosaidia wananchi kufikisha matatizo na kero zao kwa urahisi .
Ameahidi kutoa ushirikiano kwa kupitia wananchi kuhakikisha mradi huo unafanikiwa kwa kiasi kikubwa. Ameishukuru Aitel Tanzania kwa mchango wake wa kuruhusu mitambo ya Radio UVINZA F.M kufungwa katika minara hiyo.
Akizungumza Mkurugenzi wa UVINZA F.M bwana AYOUB KALUFYA amewaasa wanawake watumie fursa ya radio hiyo kuweza kutatua matatizo yao kwani radio hiyo ipo kwa ajiri yao pia kudumisha amani na mshikamano baina yao.
Vilevile amelishukuru Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni- UNESCO kwa kushirikiana na Shirika jingine la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo –UNDP, Katika kuhakikisha mradi huo untekelezwa katika wilaya ya uvinza kama ndoto yake kutetea haki za akina mama.
Katika uzinduzi huo kumeambatana na mafunzo ya watangazaji watakao endesha radio hiyo kwa kipindi cha majaribia, Mkurugenzi huyo amesisitiza wanawke kujitokeza kwa wingi kusaidia kukuza vipaji vyao na kujikwamua kimaisha kuepukana na mitazamo duni baina yao kuwa wamesahaulika katika jamii.
Mafunzo hayo yameendeshwa na Bi ROSE HAJI kwa wanafunzi ishirini kwa wiki moja kwa lengo la kuwajengea uwezo na jinsi yakutayarisha vipindi kwa mbinu ya UVINZA FM ikiwa ni mchakato wa kudumisha amani kupitia vyombo vya habari.
MWISHO
Na Winfrida Bwire, Kigoma.
ReplyDeleteMikakati ya uchumi.
Halmashauri za Wilaya na Manispaa zimetakiwa kuandaa mikakati madhubuti ya kuondoa umasikini katika jamii kwa kutumia rasilimali zinazowazunguka Wananchi wa maeneo husika.
Hayo yameelezwa na Mratibu msaidizi wa Mradi wa kukuza uchumi unaotekelezwa katika Mikoa ya Kigoma na Pwani, Girson Ntimba ambapo amedai Wananchi wanategemea mikakati yenye ubora kwa ajili ya kujenga msingi imara wa kupambana na umasikini katika jamii na hivyo kukuza uchumi.
Mikakati hiyo inatarajiwa kuwa chachu ya kuanzisha miradi ya maendeleo itakayotumika kuinua uchumi kwa kutumia mazao na rasilimali nyingine zilizopo katika jamii kama vile mazao ya kilimo na madini ambayo yanapatikana kwa wingi mkoani Kigoma.
Amesema mikoa hiyo ilichaguliwa kutokana na kiwango kikubwa cha umasikini wa kipato unaowakabili wakazi wake ambao wanadaiwa kuwa na hali ngumu ya maisha inayopelekea wengi kushindwa kuhudumia familia zao hususan katika kukidhi mahitaji muhimu ya elimu na matibabu.
Ntimba alisema ili kuinua uchumi wa Wananchi ni budi kila mmoja akatoa mchango wake katika kudumisha ushirikiano utakaopelekea kukuza uchumi wa Wananchi bila kujali itikadi na maeneo wanayoishi.
Alisema ili kukuza uchumi, wadau hawana budi kuwainua wakulima kiuchumi ili walime kilimo bora na chenye tija kinachofuata kanuni bora kuanzia kuandaa mashamba hadi kuvuna mazao yanapokomaa.
Amewataka Viongozi wa Wilaya zinazotekeleza mikakati hiyo kuhakikisha wanasimamia vema maendeleo ili wengine wakajifunze katika mikoa hiyo ya Kigoma na Pwani kwa manufaa ya Watanzania wote.
Mikakati hiyo inatakiwa kutekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya za Kigoma, Kibondo, Mkuranga, Mafia na Rufiji ambapo pia Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji itanufaika na mikakati hiyo ya maendeleo kwa maslahi ya Jamii.
Mwisho.
WIMBI LA MIFUGO MINGI KUINGIA KATIKA VIJIJI VYA WILAYA YA UVINZA
ReplyDeleteNa. Winfrida Bwire, Nguruka
Wananchi katika kata za Mganza , Itebula, Mtego wa noti na Nguruka katika wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma, wamelalamikia wimbi la mifugo mingi kuingia katika vijiji vyao na katika maeneo ya hifadhi kutoka mikoa jirani hali ambayo, inaathiri mazingira na kusababisha migogoro ya wakulima na wafugaji.
Wananchi hao wameeleza kero hiyo wakati wakijadili sera ya maendeleo ya jamii kupitia asasi ya maendeo ya Nguruka( Nguruka Development Agent-NDA. kwa ufadhili wa Fundation for Civil Society kuwa kumekuwa na wimbi kubwa la maelfu ya mifugo kuingia katika misitu na maeneo ya mashamba ya wakulima, hali ambayo kama itaachwa katika kipindi cha muda mfupi itasababisha matatizo katika jamii ikiwa ni pamoja na uharibifu wa misitu kutokana na ukataji miti hovyo.
Akisoma risala ya washiriki wa mafunzo ya sera ya taifa ya maendeleo ya jamii kwa viongozi wa vijiji, viongozi wa dini , watu maarufu na wananchi kutoka kata ya Mganza, mshiriki wa mafunzo hayo Simba Lugumbwa amesema pamoja na changamoto ya kuingia kwa mifugo, tarafa ya Nguruka inakabiliwa na tatizo la uharibifu wa mazingira kutokana na kilimo cha tumbaku na uvuvi haramu katika maziwa ya Nyamagoma na Sagara .
Wamesema pamoja na serikali kupiga marufuku bado mifugo hiyo inaingia kwa kasi huku wafugaji hasa toka mikoa ya Simiyu na Shinyanga wakidai wanaipitisha mifugo hiyo kuelekea mkoani Katavi jambo ambalo limebainika kuwa sio sahihi.
Hivi karibuni mkuu wa Wilaya ya Uvinza Hadija Nyembo alipiga marufuku mifugo kuingia katika wilaya hiyo, ambapo hata hivyo kutokana na kuwa tayari imeingia, vijiji vimeweka mikakati kadhaa ya kukabiliana na wimbi hilo ikiwa ni pamoja na kutenga maeneo ya wakulima na wafugaji na kuirudisha ilikotoka mifugo inayoingia hivi sasa
Afisa mtendaji wa kijiji cha Kasisi , moja ya vijiji vilivyoathiriwa na mifugo , Ali Kisila amesema baada ya Serikali kutoa maelekezo juu ya mifugo , hivi sasa wafugaji wote wanaoingia wanarejeshwa walikotoka na kwamba ni wafugaji walioingia mwaka mmoja uliopita ndio wameruhusiwa na kupatiwa maeneo ya katika vijiji .
Akizungumzia mafunzo hayo mratibu wa asasi ya Nguruka Development Agent, Maisha Salum , amesema Asasi hiyo iliomba fedha Foundation For Civil Society ili kusaidia kutoa elimu kwa jamii katika eneo hilo juu ya sera ya maendeleo ya jamii kwa lengo la kukuza uwajibikaji na kila mtu kutumia fursa zinazomzunguka kujiendeleza .
Katibu wa asasi hiyo isiyo ya kiserikali Stanford Chamgeni alisema, katika asasi hiyo, makundi matatu katika jamii yanapewa kipaumbele kuyahudumia , kulingana na mahitaji yake , makundi hayo ni wazee wasiojiweza , watoto yatima na akinamama ambao wamekuwa wakiathirika sana kutokana na matatizo ya uzazi, ambapo amesema kwa kushirikiana na kituo cha afya Nguruka wameanzisha mpango utakaosaidia kupunguza vifo vya watoto na akinamama.
Kwa upande wake afisa maendeleo ya jamii katika Halmashauri ya Kigoma Alberto Ndumbala aliyeendesha mafunzo hayo, amesema kupitia sera ya maendeleo ya jamii, wananchi wanaweza kujikwamua kwa kuwa sera imetoa fursa kwa jamii kutumia raslimali zinazowazunguka kujiendeleza .
Amesema tatizo kubwa linalowakabili wananchi ni kutoifahamu sera, hali ambayo inawafanya washindwe kuitumia na kwamba kupitia mafunzo kama hayo , anaamini jamii itaanza kuitumia .