Tuesday, October 1, 2013

UZINDUZI NRA KATA YA MKONGORO



CHAMA cha National Reconstruction Alliance (NRA) kimezindua kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata ya Mkongoro Halmashauri ya wilaya kigoma huku mgombea wake Fadhili Kiswaga akiahidi kupigania kuboreshwa kwa mazao ya kahawa, nanasi na michikichi ili kuwafanya wakulima wa mazao hayo kuondokana na umasikini.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara wa uzinduzi wa kampeni hizo uliofanyika kwenye kijiji cha Mkongoro, Mgombea huyo wa NRA alisema kuwa ni jambo la kusikitiisha kuona kijiji cha Mkongoro kikiwa na sifa kubwa ya kulima nanasi zinazipendwa huku wakulima wake wako na hali mbaya kwa umasikini.

Alisema kuwa hali hiyo ya wakulima wa mazao hayo inachangiwa kwa kiasi kikubwa na viongozi waliochaguliwa kushindwa kusimamia utekelezaji wa miradi ya kuwaondiolea umasikini wananchi na badala yake viongozi hao kujali maslahi yao.

“ndugu zangu sote tunajua kata ya Mkongoro inafahamika kwa kilimo cha mazao ya chikichi,kahawa na mananasi lakini wakulima wa mazao hayo ukiwaangalia wako hoi kwa umasikini, hakuna wa kuwatetea ili kuboreshewa kwa miundo mbinu ya masoko waweze kuuza mazao yao na kupata faida, Halmashauri inakusanya kodi kila siku lakini haijali kuweka mazingira mazuri kwa wakulima hao,”

Nichagueni niwe mtumishi wenu, nikopesheni kura name nitawalipa maendeleo, nitakuwa kiongozi ambayo atasimama badala ya watu siyo kama wale walioweka ubinfsi mbele na kunagalia maslahi yao, mmewatuma halmashauri wakafanyeni kazi lakini wao wanafanya kinyume chake,”alisisitiza Kiswaga.

Awali mwenyekiti wa chama cha NRA mkoa kigoma, alisema kuwa chama hicho Khalif Khalfani milembe alisema kuwa chama hicho kimemsimamisha Kiswaga kwenye uchaguzi huo kutokana na umahiri wake kiutendani wakiamini kuwa atakuwa msaada mkubwa kwa maendeleo ya wananchi wa kata ya Mkongoro.

Milembe alisema kuwa wananchi wa kata hiyo kutomchagua Kiswaga ni sawa na kuacha dhahabu izolewe na maji na ndiyo maana chama hicho pia kilimfanya kiongozi huyo kuwa Katibu Mwenezi wake wa Taifa kutokana na umahiri huo wa utendaji wake.

Akieleza kufanyika kwa uchaguzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya kigoma, Miriam Mbaga alisema kuwa uchaguzi huo unafanyika kufuatia kifo cha diwani wa kata hiyo, Sospeter Laurent na kwamba uchaguzi huo utafanyika Februal 9 mwaka huu.

Mbaga alisema kuwa tume ya uchaguzi ilizindua ratiba ya kampeni Januari 16 mwaka huu hadi Februari 8 ambapo jumla ya vyama saba vinatareajiwa kushiriki uchaguzi huo vikiwemo CCM, CHADEMA, CUF, NCCR – Mageuzi, NRA, NLD na DP.
  



makamu wa Raisi wa muungano wa vilabu vya waandishi wa habari nchini (UTPC), Jane Mihanji akisisitiza jambo katika mkutano mkuu wa mwaka wa Kigoma Press Club KGPC (kati kati) ni Mwenyekiti wa Kigoma Press Club, Deo Nsokolo

No comments:

Post a Comment