mkuu wa mkoa Kigoma Issa Machibya akipokea msaada wa moja ya mashine tano za upasuajia zenye thamani ya shilingi milioni 100 kwa ajili ya vituo vitano vya afya mkoani Kigoma kutoka kwa Brigita Steffan (Katikati) Mke wa mkurugenzi wa miradi wa shirika la World Lung Foundation Staffan
Bergstrom (kulia) katika hafla ya kukabidhi mashine hiyo kwa ajili ya Kituo cha Afya Ujiji Manispaa ya Kigoma Ujiji
Mkuu wa mkoa kigoma Issa Machibya akikata utepe kuashiria kuzinduliwa kwa huduma za upasuaji katika kituo ch afya Ujiji manispaa ya Kigoma Ujiji kushoto ni Mkurugenzi wa Shirika la World Lung Foundation Steffan Bergstrom.
SHIRIKA la Wolrd Lung Foundation lenye makao yake makuu nchini Marekani
limetoa msaada wa vifaa vya upasuaji kwa ajili ya kituo cha afya cha
Ujiji
manispaa ya Kigoma Ujiji ili kusiadia upasuaji kwa kina mama wajawazito
wanaoapata matatizo wakati wa kujifungua.
Vifaa hivyo vyenye thamani ya shilingi milioni 100 vilikabidhiwa kwa Mkuu
wa mkoa Kigoma,Issa Machibya na Brigita Staffan mke wa Mkurugenzi wa miradi
wa shirika hilo hapa nchini, Staffan Bergstrom.
Akikabidhi wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa hivyo Mkurugenzi wa miradi wa
World Lung Founation nchini, Staffan Bergstrom alisema kuwa ni wazi kuanza
kutumika kwa vifaa hivyo itakuwa mkombozi mkubwa kwa kina mama ambao upata
matatizo wakati wa kujifungua na wakati mwingine kufa.
Alisema kuwa shirika hilo limetoa mchango huo ikiwemo ni sehemu ya pato la
Meya wa Jiji la London, Peter Bloomber ambaye aliamua kujitolea sehemu ya
pato lake kwa ajili kusaidia matibabu ya kina wanaopata matatizo wakati wa
kujifungua.
Akipokea vifaa hivyo Mkuu wa mkoa kigoma Issa Machibya alisema kuwa
kutolewa kwa vifaa hivyo na kutumika katika kituo hicho cya afya ujiji
kutasaidia kupunguza kama siyo kumaliza tatizo la vifo vya kina mama
wakati wa kujifungua na itakuwa inatimiza lengo la nne la malengo ya
millennia.
Alisema kuwa ni wazi kufungwa kwa vifaa hivyo katika kituo hicho cha afya
kutapunguza msongamano katika hospitali ya Rufaa ya Maweni ambayo ilikuwa
hospitali pekee iliyokuwa ikitegemewa kwa upasuaji na wakazi wa manispaa ya
Kigoma Ujiji.
Baadhi ya kina mama waliohudhuria hafla hiyo wamesema kuwa kufungwa kwa
mashine ya upasuaji kwenye kituo hicho cha afya kutapunguza usumbufu wa
kutegemea hospitali ya maweni ambayo kwao ilikuwa ni hospitali pekee
iliyokuwa ikifanya upasuaji hapa mjini.
Mtendamema Bandora na Hamisa Kassim wakazi wa Ujiji mjini hapa walisema
kuwa kufungwa kwa mashine hizo ni mkom bozi kwao na wametoa wito kwa kina
mama wajawazito kutumia vituo vya afya kwa ajili ya kwenda kujifungulia
badala ya kujifungulia nyumbani au kwa wakunga.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment