Saturday, November 17, 2012

MAFUNZO YA IJ KIGOMA

Mwandishi wa habari Mkongwe nchini Deodatus Mfugale akisisitiza jambo wakati akiendesha mafunzo ya uandishi wa habari za uchunguzi kwa waandishi wa habari wanachama wa chama cha waandishi wa habari mkoa kigoma KGPC yaliyoendeshwa kwa uwezeshaji wa Muungano wa vilabu vya waandishi wa habari nchini (UTPC) - Picha na Fadhili Abdallah




WAANDISHI wa habari mkoani Kigoma wametakiwa kuandika habari za uchunguzi zitakazozingatia maadili na kuwa na maslahi kwa jamii badala ya kutumia uandishi wa habari za uchunguzi kama nyenzo ya kulipiza kisasi.



Mwandishi wa habari mkongwe nchini, Deodatus mfugale alisema hayo wakati wa mafunzo ya siku sita ya uandishi wa habari za uchunguzi kwa waandishi wa habari wanachama wa chama cha waandishi wa habari mkoa kigoma.


Mfugale alisema kuwa katika kuandika habari za aina hiyo waandishi wa habari wanapaswa kuzingatia hoja zinazoigusa jamii na ambazo haziendi sawa na kwamba uandishi wa habari wa aina hiyo utakuwa na maana kubwa kwa jamii.


Hata hivyo Mfugale alisema kuwa licha ya vyombo vingi vya habari nchini kujisifu kwamba vinaandika habari zilizofanyiwa uchunguzi wa kina bado vingi kati yao havijafikia mahali pa kuandika habari za uchunguzi ambazo zinahitajika kimaadili huku nyingi ya habari hizo zikiacha maswali.


Wakizungumza katika mafunzo hayo waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wanaoshiriki mafunzo hayo wamelalamikia kutokuwepo kwa uwezeshaji kutoka vyombo wanavyofanyia kazi na hivyo kushindwa kufanya kazi ya uandishi wa habari za uchunguzi na kubaki kuandika habari za matukio.


Magreth Magosso mwandishi wa habari wa gazeti la jamb oleo alisema kuwa sambamba na kutokuwepo kwa uwezeshaji vyombo vingi vya habari nchini haviko tayari kuwapatia waandishi wao vitendea kazi na hivyo kufanya kazi ya uandishi wa habari kwa waandishi wa habari hasa wa mikoani kufanya kazi katika mazingira magumu.


Awali Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoa kigoma, deo Nsokolo alisema kuwa jumla ya waandishi wa habari 18 wnaatarajia kushiriki mafunzo hayo na kwamba kufanyika kwa mafunzo hayo kutatoa nafasi na kuwapa uzoefu wa utendaji kazi waandishi chipukizi.


Nsokolo alisema kuwa pamoja na mambo mengine mafunzo hayo yanalenga kuwakumbusha waandishi wa habari umuhimu wa kuzingatia maadili, kuwahamasisha kuandika habari za uchunguzi na kuzingatia uzalendo katika kufanya kazi za habari za uchunguzi.


Mwisho.
 

No comments:

Post a Comment