Mwandishi wa habari Mkongwe nchini Deodatus Mfugale akisisitiza jambo wakati akiendesha mafunzo ya uandishi wa habari za uchunguzi kwa waandishi wa habari wanachama wa chama cha waandishi wa habari mkoa kigoma KGPC yaliyoendeshwa kwa uwezeshaji wa Muungano wa vilabu vya waandishi wa habari nchini (UTPC) - Picha na Fadhili Abdallah
WAANDISHI wa
habari mkoani Kigoma wametakiwa kuandika habari za uchunguzi zitakazozingatia
maadili na kuwa na maslahi kwa jamii badala ya kutumia uandishi wa habari za
uchunguzi kama nyenzo ya kulipiza kisasi.
Mwandishi wa
habari mkongwe nchini, Deodatus mfugale alisema hayo wakati wa mafunzo ya siku
sita ya uandishi wa habari za uchunguzi kwa waandishi wa habari wanachama wa
chama cha waandishi wa habari mkoa kigoma.
Mfugale alisema
kuwa katika kuandika habari za aina hiyo waandishi wa habari wanapaswa
kuzingatia hoja zinazoigusa jamii na ambazo haziendi sawa na kwamba uandishi wa
habari wa aina hiyo utakuwa na maana kubwa kwa jamii.
Hata hivyo
Mfugale alisema kuwa licha ya vyombo vingi vya habari nchini kujisifu kwamba
vinaandika habari zilizofanyiwa uchunguzi wa kina bado vingi kati yao
havijafikia mahali pa kuandika habari za uchunguzi ambazo zinahitajika
kimaadili huku nyingi ya habari hizo zikiacha maswali.
Wakizungumza
katika mafunzo hayo waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari
wanaoshiriki mafunzo hayo wamelalamikia kutokuwepo kwa uwezeshaji kutoka vyombo
wanavyofanyia kazi na hivyo kushindwa kufanya kazi ya uandishi wa habari za
uchunguzi na kubaki kuandika habari za matukio.
Magreth Magosso
mwandishi wa habari wa gazeti la jamb oleo alisema kuwa sambamba na kutokuwepo
kwa uwezeshaji vyombo vingi vya habari nchini haviko tayari kuwapatia waandishi
wao vitendea kazi na hivyo kufanya kazi ya uandishi wa habari kwa waandishi wa
habari hasa wa mikoani kufanya kazi katika mazingira magumu.
Awali Mwenyekiti
wa chama cha waandishi wa habari mkoa kigoma, deo Nsokolo alisema kuwa jumla ya
waandishi wa habari 18 wnaatarajia kushiriki mafunzo hayo na kwamba kufanyika
kwa mafunzo hayo kutatoa nafasi na kuwapa uzoefu wa utendaji kazi waandishi
chipukizi.
Nsokolo alisema
kuwa pamoja na mambo mengine mafunzo hayo yanalenga kuwakumbusha waandishi wa
habari umuhimu wa kuzingatia maadili, kuwahamasisha kuandika habari za
uchunguzi na kuzingatia uzalendo katika kufanya kazi za habari za uchunguzi.
Mwisho.