Na Fadhili Abdallah,Kigoma
JESHI la polisi mkoani Kigoma linamtafuta mwanafunzi wa shule ya msingi Rwiche katika halmashauri ya wilaya Kigoma Rehema Issa ambaye alijifungua mtoto na kumtupa chooni jambo lililosababisha kifo cha mtoto huyo.
Kaimu Kamanda wa polisi mkoa Kigoma, Francis Mwakabana amesema mjini Kigoma kwamba baada ya mwanafunzi huyo kujifungua mtoto huyo ambaye alimtupa katika choo cha shimo cha shule ya msingi Nyangwe akiwa hai na baadaye kuokolewa kutoka katika choo hicho na wanafunzi wa shule hiyo.
Hata hivyo Kamanda huyo wa polisi mkoa Kigoma amesema kuwa kichanga hicho kilifariki muda mfupi baada ya kuokolewa kwenye choo hicho cha shule na mwili wake umehifadhiwa katika hospitali ya mkoa Kigoma Maweni huku jitihada za jeshi hilo kumsanga mwanafunzi huyo zikiendelea.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment