Jaji wa mahakama kuu kanda ya Tabora Sam Mpaya Rumanyika akikagua gwaride la askari wa kikosi cha kutulia ghasia ikiwa ishara ya kuanza kwa kikao cha mahakama kuu mkoani Kigoma
Jaji wa mahakama kuu kanda ya Tabora Sam Mpaya Rumanyika akipokea salamu za utii kutoka kwa kikosi cha askari wakutuliza ghasia (Hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa kikao cha mahakama kuu kanda ya Tabora mkoani Kigoma (kulia) ni Kamanda wa polisi mkoa Kigoma Fraisser Kashai na nyuma ni watumishi mbalimbali wa serikali wakiongozwa na Mkuu wa mkoa kigoma Issa machibya
Sunday, May 19, 2013
WADAU WA HABARI KIGOMA
Wadau wa habari mkoani Kigoma wakifuiatilia hotuba mbalimbali zilizokuwa zikitolwa siku ya maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari mkoani Kigoma.
Kamanda wa polisi Fraisser Kashai ambaye alikuwa mgeni rasmi siku ya maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari mkoani Kigoma akitoa hotuba yake kwa washiriki wa maadhimisho hayo
Kamanda wa polisi Fraisser Kashai ambaye alikuwa mgeni rasmi siku ya maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari mkoani Kigoma akitoa hotuba yake kwa washiriki wa maadhimisho hayo
SIKU YA UHURU WA HABARI NCHINI
Na Fadhili
Abdallah,Kigoma
Wadau wa habari mkoani Kigoma wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni Rasmi Kamanda wa polisi mkoa Kigoma Fraisser Kashai siku ya maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari mkoani Kigoma
Waandishi wa habari kutoka chama cha waandishi wa habari mkoani Kigoma wakiwa katika picha ya pamoja na kamanda wa polisi mkoa Kigoma Fraisser kashai mwenye kofia waliokaa wakati wa maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari mkoani Kigoma (Picha zote na Fadhili Abdallah)
Na Mwandishi wetu, Kigoma
WAANDISHI wa
habari mkoani Kigoma wametakiwa kutumia kalamu zao kwa kuzingatia misingi ya uandishi wa habari kwani zikitumika vizuri zinaweza kuwa
chachu na mchango mkubwa katika kuleta maendeleo ya jamii na kwamba kinyume
chake kalamu za waandishi zinaweza kugeuka risasi na kuleta maafa makubwa kwa
jamii.
Diwani wa kata ya
Mwanga Kaskazini, Francis Mangapi alisema hayo katika kilele cha maadhimisho ya
siku ya uhuru wa vyombo vya habari mkoani Kigoma yaliyoratibiwa na chama cha
waandishi wa habari mkoani humo (KGPC).
Mangapi alisema
kuwa tumeshuhudia maeneo mbalimbali ambapo waandishi wametumika vizuri kumekuwa
na maendeleo makubwa na jamii imehamasika katika kujieleta maendeleo lakini
mahala ambapo waandishi wametumika vibaya kumekuwa na matatizo makubwa makubwa.
Akichangia
kuhusiana na jambo hilo Mfanyabiashara maaruru wa mjini Kigoma Miforo
Mpozemenya alisema kuwa waandishi wa habari wasikubali kutumiwa na wanasiasa
ama makundi mbalimbali kwa faida zao badala yake wajikite katika kufanya
kazi kwa kuzingatia maslahi ya jamii na kufuata maadili ya taaluma yao.
Akizungumza
katika maadhimisho hayo Kamanda wa polisi mkoa Kigoma, Fraisser Kashai ambaye
alikuwa mgeni rasmi alisema kuwa pamoja na changamoto mbalimbali zilizopo baina
ya waandishi na jeshi lake lakini waandishi wa habari wamekuwa mchango mkubwa
katika kufanikisha mambo mbalimbali ya kiutendaji ndani ya jeshi la polisi.
Kashai alisema
kuwa jeshi lake litaendelea kutoa msaada na kushirikiana na vyombo vya habari
kwa kadri iwezekanavyo na kwamba kama kuna kutoelewana mahali baina yao ofisi
yake iko wazi muda wote kwa ajili ya majadiliano na kuzungumza namna gani ya
kuweza kufanya kazi pamoja.
Awali Mwenyekiti
wa chama cha waandishi wa habari mkoa kigoma, Deogratius Nsokolo, matukio ya
hivi karibuni ya kuuawa kwa mwandishi wa habari,Daudi Mwangosi wa Iringa, Issa
Ngumba wa Kibondo mkoani Kigoma na kuteswa na kutobolewa jicho kwa Mwenyekiti
wa jukwaa la wahariri Tanzania, Absolom Kibanda kunawafanya waandishi wa habari
watafakari namna ya utekelezaji wa majukumu yao.
Hata hivyo
Nsokolo alisema kuwa matukio hayo badala ya kuwarudisha nyuma na kuwavunja moyo
badala yake vimewapa ari , ujasiri na mbinu mpya waandishi wa habari
katika kuendeleza majukumu yao lakini pia kufichua mambo
mabaya ambayo yanafanywa na watu wachache huku mambo hayo ikiacha jamii kubwa
ya Watanzania ikiteseka.
Mwisho.
WANAOHAMISHWA KIBIRIZI WALALAMIKIA FIDIA KUCHELEWA
Na Fadhili Abdallah,Kigoma
wafanyabiashara na wananchi waliokuwa
wakiishi na kufanya shughuli zao katika eneo la bandari ndogo ya kibirizi Manispaa
ya kigoma ujiji, wamelalamikia hatua ya manispaa hiyo kuchelewesha kuwalipa
malipo yao ya fidia na kuwazuia kufanya shughuli zozote za kujiingizia kipato.
Wakizungumza katika mahojiano maalum
na gazeti wananchi hao wamesema kuwa baada
ya kufanywa tathmini ya upanuzi wa bandari ndogo ya Kibirizi manispaa ya
Kigopma Ujiji zaidi ya mwaka mmoja uliopita lakini
mpaka sasa hakuna kilichofanyika.
Mmoja wa wananchi hao Patrick Ntahondi
alisema kuwa amekuwa na hali ngumu kimaisha kwani hawezi kufanya lolote katika
eneo lake kwa sasa kwa sababu watu wengi wameshahama na kuhamisha shughuli zao
lakini wao hawaelewi mambo yakoje na kuwawia ngumu kuendesha maisha yao.
Naye Jasmine Katekwe alisema kuwa
ana nyumba yake katika eneo hilo ambayo alikuwa akiitumia kupangisha
wafanyabishara kuhifadhi mizigo yao na pia kuwapa eneo la kukaushia samaki na
dagaa lakini serikali imesimamisha shughuli za biashara na hali kiuchumi kwake
imekuwa ngumu.
Sambamba na hilo alisema kuwa anashindwa
kufanya marekebisho yeyote katiuka nyumba yake kutokana na serikali kueleza
kwamba tayari tathmini imeshafanyika ambapo wameiomba serikali kuingilia kati
na kuwaruhusu waendelee na shughuli za kuwaingizia kipato na makazi.
Akizungumzia jambo hilo Naibu Meya
wa Manispaa ya Kigoma Rashidi Ruhonvya amesema
kuwa kuchelewa kulipwa fidia kwa wananchi wa eneo hilo kumetokana na kukosewa
kwa tathmini ya awali baada ya kuwepo kwa baadhi ya wananchi ambao
hawakujumuishwa licha ya maeneo na vibanda vyao kubainishwa.
Alisema kuwa tayari muhakiki
ameshafika na anaipitia upya repoti ya tathmini kuona kama kuna itilafu mahali
na kwamba baada ya kufanyiwa marekebisho kwa itililafu zilizojitokeza malipo ya
watu hao yatafanywa haraka iwezekanavyo na kwani uhakiki huo umefikia hatua ya
mwisho.
Hata hivyo Ruhovya ametoa wito kwa
watu wote waliokuwa wakiishi na kufanya shughuli mbalimbali katika eneo hilo kusitisha
mambo hayo wasubiri kulipwa fidia zao na kutafuta maeneo mengine kwa ajili ya
makazi na shughuli zao.
Mwisho.
ILI
kuhakikisha wanawatumia watoto wao katika shughuli zao za kiuchumi badala ya
kuwa shuleni imebainika kuwa wazazi wengi katika vijiji mbalimbali vya wilayani Kibondo wanakaidi kwa makusudi kuwalipia ada na
michango mbalimbali watoto waliofaulu na kuchaguliwa kujiunga na masomo ya sekondari wilayani
humo.
Uchunguzi
uliofanywa na gazeti na kuthibitishwa na ngazi mbalimbali za uongozi wa
kiserikali na kijamii imethibitisha kwamba
vitendo hivyo vimefanya uongozi wa shule za sekondari katika wilaya hiyo
na serikali za vijiji na kata kutumia muda mrefu katika kuhangaika kuwaokoa
watoto hao na vitendo vya wazazi wao.
Akithibitisha
kuhusiana na hilo Mkuu wa shule ya sekondari ya kutwa ya Kumgogo tarafa ya
Mabamba wilayani humo, Adolf Tuseko alisema kuwa vitendo vya wazazi kukaidi
kuwalipia ada watoto kwa makusudi vimechukua nafasi kubwa ya shughuli za
utawala shuleni hapo zaidi ya shughuli za kitaaluma.
Mkuu huyo wa
shule alithibitisha kwamba wazazi wanatumia hila ya kutokuwa na fedha za
kuwalipia watoto wao ili watoto hao watakaporudishwa nyumbani iwe rahisi kwao
kuwatumia kwa shughuli za kufanya vibarua kwenye mashamba na biashara kwenye
magulioa.
Alisema kuwa
kufuatia hali hiyo wanalazimika kulipeleka suala hilo katika uongozi wa kata
ambapo majina ya wazazi ambao wanachukua muda mrefu kutolipa michango hiyo
hupelekwa huko na mtendaji wa kata na baraza la maendeleo la kata ndiyo husimamia
hilo.
Akizungumzia
kuhusiana na hilo Mwalim Mkuu wa shule ya Msingi Mkarazi, Asumwisye Peter
alisema kuwa pamoja na madai ya kipato
kidogo cha wazazi lakini wazazi wengi hawana mwamko wa elimu na ndiyo maana
hawaoni umuhimu wa watoto wao kuendelea na masomo ya sekondari.
Alisema kuwa
kabla ya ujenzi wa sekondari za kata watoto wengi walikuwa wakiishia darasa la
saba na wazazi walikuwa wakipata nafasi ya kuwatumia watakavyo na kuwafanya
ndiyo chanzo cha kuingiza mapato kwa ajili ya kuendesha familia kutokana na
kutumika kwenye kufanya kazi za vibarua.
Anasema kuwa
wakati mwingine hasa wakati wa magulio au wakati wa kilimo watoto wengi
hutolewa shuleni na kwenda kufanya kazi kwenye mashamba au masoko na hiyo si
kwa shule za msingi tu bali hata kwa shule za sekondari na imekuwa ni tatizo
kubwa kati ya shule na jamii inayozunguka shule hizo ambao watoto wao wanasoma
hapo.
Kwa upande
wake mmoja wa wazazi walioongea na gazeti hili, Method Kalumanzila
alithibitisha kwamba kitendo cha wazazi kutolipa ada na pia kuwatoa watoto
shule kwa ajili ya kwenda kufanya vibarua imekuwa tatizo sugu na kikubwa ni
mwamko mdogo wa wazazi katika elimu na hali duni ya kipato kwa wazazi.
Naye Mzazi
mwingine, Magreth Sunzu mfanyabiashara katika soko la Mabamba alisema kuwa wazazi hawaoni umuhimu wa watoto wao
kuendelea na masomo ya sekondari kwa sababu baada ya miaka minne ya masomo
wengi huambilia alama sifuri (Division Zero) na kubaki nyumbani kama wenzao
walioishia darasa la saba.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Kigoma, Leopold Ulaya alithibitisha matatizo hayo mawili
kuikabili wilaya yake na kusema kuwa wamo katika mchakato wakuona wafanye nini
kukabiliana na hali hiyo lakini kwa sasa uongozi wa kata umepewa mamlaka ya kuwachukulia
hatua wazazi kwa kuwafikisha kwenye baraza la kata na kuwatoza faini.
Sambamba na
hilo alisema kuwa wanatarajia kutembelea halmashauri ambazo zinachamoto kama ya
kwao ili kuona namna gani wanafanya kukabiliana na hali hiyo lakini pia
wanawaza namna ya kutunga sheria ndogo za halmashauri ambazo zitawabana na
kuhakikisha kwamba wanalipa michango ya watoto wao na pia kuhakikisha kwamba
watoto wao kuhudhuria masomo.
Mkuu wa
wilaya kibondo kwa upande wake alisema kuwa utoro kwa wanafunzi wa sekondari
kuacha masomo na kwenda kufanya shughuli za biashara na vibarua ni tatizo kubwa
lakini pia suala la wazazi kukataa kulipia gharama za masomo ya watoto wao ni
tatizo lingine ambayo kwa pamoja wanayatarajia kuyafanyia kazi katika kikao cha
wadau wa elimu wanachotarajia kuitisha.
Mwisho.
Friday, April 12, 2013
UZINDUZI MINARA YA TIGO KASULU
Mkuu wa wilaya Buhigwe, Charles Gishuli akikata utepe kuzindua matumizi ya mnara wa kampuni ya simu ya mkononi ya Tigo anayeshuhudia (kushoto) ni meneja wa tigo kanda ya ziwa Joseph Mutalemwa.
Meneja wa kampuni ya Tigo kanda ya ziwa Joseph Mutalemwa akizungumza katika uzinduzi wa minara ya kampuni hiyo wilayani Kasulu.(Picha na Fadhili Abdallah)
Na Fadhili
Abdallah,Kigoma
KAMPUNI ya
simu ya mkononi ya tigo imezindua mpango wa uwekaji wa
minara mipya ya mawasiliano ili kuongeza wigo wa huduma zake kufikia wateja
hadi wale wa vijijini na kufanya mawasiliano ya kampuni hiyo kupatikana wakati
wote.
Meneja wa
kanda ya ziwa wa Tigo, Joseph Mutalemwa akizungumza kwa niaba ya Meneja Mkuu wa
kampuni hiyo, Diego Guiterez alisema kuwa katika awamu ya kwanza ya mpango huo
utaanzia kwa mikoa ya Kigoma, Kagera,Tabora,Mwanza na Mara.
Amesema kuwa
katika awamu hiyo jumla ya minara mipya 300 itajengwa ambapo kati hiyo minara 141 itajengwa kanda ya ziwa huku mkoa
kigoma itajengwa jumla ya minara 24 na tayari minara mitatu imeshaanza kufanya
katika mradi unaotarajiwa kukamilisha mweze Septemba mwaka huu.
katika hatua nyingine kampuni ya tigo imekabidhi jumla ya vitabu 1000 vya masomo ya sayansi vyenye thamani ya shilingi milini saba kwa shule ya msingi Nyaminkunga wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma ili kukabiliana na upungufu wa vitabu unaoikabili shule hiyo.
Akizungumza katika
hafla ya kukabidhi vifaa hivyo iliyoenda sambamba na uzinduzi wa mnara wa
mawasiliano mjini Kasulu, Meneja wa Tigo Kanda ya ziwa Joseph Mutalemwa alisema
kuwa msaada huo ni sehemu ya mpango mkakati wa kampuni hiyo katika kusaidia
huduma za kijamii.
Alisema kuwa
vitabu hivyo 1000 vya masomo ya sayansi kwa darasa la nne hadi la sita
vinalenga kuchochea wanafunzi katika shule hiyo kupenda masomo ya sayansi
ambayo ndiyo msingi wa mainjinia na madokta.
Akizindua
kuanza kwa matumizi ya minara hiyo mipya na kukabidhi vitabu Mkuu wa mkoa
kigom, Issa Machibya amewataka wananchi wa mkoa huo kutumia uwepo wa
mawasiliano ya simu za mkononi kuboresha shughuli zao za kiuchumi.
Katika hotuba
iliyotolewa kwa niaba yake na Mkuu wa wilaya Buhigwe, Charles Gishuli alisema
kuwa simu za mkononi zimekuwa na matumizi mengi na muhimu kwa maisha ya kila
siku ya mwanadamu badala ya kuishia kupiga simu na kutuma ujumbe mfupi wa
maandishi.
Mwisho.
VIONGOZI UWT WATEMBELEA BURUNDI
Picha mbalimbali za viongozi wa Umoja wa wanawake wa CCM mkoa Kigoma walipofanya ziara katika mkoa wa Ruyigi nchini Burundi kutembelea shughuli za chama cha CNDD - FDD cha nchini Burundi.(Picha na Fadhili Abdallah)
Na Fadhili Abdallah,
Ruyigi Burundi
UJUMBE wa viongozi wa watano wa jumuia ya umoja wa wanawake
wa CCM (UWT) umefanya ziara ya ujirani mwema nchini Burundi na kutoa mwito kwa
viongozi na wanachama wa jumuia ya wanawake wa chama tawala nchini humo CNDD –
FDD A’bakenyera Rugamba kutokubali amani
ya nchi ichezewe na kuifanya nchi hiyo kurudi vitani.
Akizungumza katika mkutano wa pamoja kati ya UWT na
A’bakenyera Rugamba Mjumbe wa baraza kuu Taifa la UWT, Josephine amesema kuwa
wanawake wanayo nafasi kubwa katika kuhakikisha kwamba wanasimamia amani
inadumishwa nchini humo.
Alisema kuwa kuvurugika kwa amani kunaathari kubwa kwa
wanawake na watoto na uzoefu huo umejionyesha katika vuta ya wenyewe kwa
wenyewe iliyomalizika nchini humo ambapo wanawake na watoto walikuwa wahanga
wakubwa wa vita.
Akizungumzia ushirikiano na mahusiano kati ya jumuia hizo
mbili Josephine ambaye ni Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Uvinza alisema kuwa
mkutano huo bado na kubadilisha mawazo lakini pia unalenga kuwapa mbinu na
mkakati viongozi wa jumuia hiyo kuifanya CNDD – FDD kuongoza nchi ya Burundi
kwa muda mrefu.
Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Taifa wa jumujia ya wanawake wa chama cha CNDD – FDD
A’bakenyera Rugamba, Yamuremiye Goreth alisema kuwa ziara hiyo imekuwa na
manufaa makubwa kwao kwani katika mkutano na majadiliano ya pamoja waliyofanya
yamewapa uzoefu wa nini cha kufanya katika siku zijazo.
Alisema kuwa moja ya mambo ambayo yamewapa mwanga namna ya
kufanya ukiacha suala la mambo ya kisiasa alisema kuwa hata suala la uchumi
linapaswa kuingizwa kwenye siasa kwa wanachama wa chama hicho kupewa nguvu za
kiuchumi kwa kuanzishiwa miradi ya kujitegemea ya kuwaingizia kipato.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha CNDD – FDD mkoa Ruyigi,
Ngerageze Egide alisema kuwa chama hicho kimeweza kuongoza kwa amani hadi sasa
baada ya Raisi Nkurunzinza kushika madaraka inatokana na kiongozi huyo kuondoa
ubaguzi katika kuunda serikali.
Egide alisema kuwa serikali ya Burundi kwa sasa inaongozwa
kwa mseto wa makabila yote kujumlishwa kwenye serikali jambo ambalo limewafanya
wananchi kulifurahia lakini pia Raisi Nkurunzinza amejitahidi kutumia
rasilimali za nchi katika utekelezaji wa miradi mbalimbali inayowagusa wananchi
moja kwa moja.
Mkutano huo wa pamoja wa vyama hivyo ulifikia maazimio ya
kuwa na safari za kila mwaka kwa
viongozi wa jumuia hizo za wanawake za CNDD – FDD na CCM kutembeleana na
kubadilisha uzoefu katika masuala ya siasa, uchumi na utamaduni.
mwisho
WATU
50 raia wa Burundi ambao waliathirika na vita vya wenyewe kwa wenyewe
nchini Burundi wame wameanzishiwa miradi ya kiuchumi ambayo itawasaidia
kuwaingizia kipato kwa ajili ya kuendeshea maisha yao.
Katibu Mtendaji wa jumuia ya wanawake wa chama cha CNDD - FDD (A’bakenyera Rugamba), Yamuremiye Goreth alisema hayoi wakati Akitoa taarifa kwa viongozi wa jumuia ya wanawake wa CCM (UWT) mkoa Kigoma waliofanya ziara ya Ujirani mwema nchini Burundi.
Alisema kuwa sehemu ya wananchi hao walikuwa askari wakati wa vita, wapo wanawake waliofiwa na waume zao ambao walikuwa wapiganaji na wazee ambao familia zao ziliteketea kwenye vita hiyo.
Goreth alisema kuwa watu hao wamepatiwa eneo la Hekta 14 ambalo wamepanda
mazao mchanganyiko ikiwemo Mananasi, Mihogo na ndizi katika eneo la
kijiji cha Nyaburondwe, tarafa ya Butaganzwa mkoa wa Ruyigi.
katika uwezeshaji huo Raisi Pierre Nkurunzinza amekipatia kikundi hicho kiasi cha Faranga milioni 6.5 sawa na zaidi ya shilingi milioni saba za Tanzania kwa ajili ya kupatiwa utaalam wa kilimo na uimarishaji wa kikundi chao.
Katibu huyo Mtendaji wa A’bakenyera Rugamba alisema kuwa serikali imechukua hatua hiyo ili kuwasaidia watu hao kutokana na athari za kijamii na kiuchumi walizopata ambazo zimepelekea kuathirika kisaikolojia.
Wakizungumzia hatua viongozi wa UWT waliokuwa kwenye ziara hiyo waliishukuru serikali ya Burundi inayoongozwa na Raisi Nkurunzinza kwa kuchukua hatua mbalimbali za kurekebisha maisha wa watu nchini humo.
Mjumbe wa baraza kuu la UWT Taifa, Josephine Hosea alisema kuwa jumuia hiyo iko pamoja na chama hicho na serikali kwa jumla katika kusaidia kwa hali na mali kuona wananchi wa Burundi wanarudia
maisha yao ya kawaida ya kabla ya vita.
BANGI YAKAMATWA IKILIMWA PORINI
Na Mwandishi Wetu, Kigoma.
zaidi ya miche elfu mbili ya bangi
imegundulika na kuteketezwa , ikilimwa katika eneo la msitu wa hifadhi
ya taifa ya akiba ya muyowosi kigosi na maeneo jirani katika wilaya ya
kibondo mkoani kigoma .
hali hiyo imegundulika wakati wa oparesheni maalum ya kusaka mashamba ya bangi iliyofanywa
na jeshi la polisi wakiongozwa na kamanda wa polisi mkoa wa kigoma
fraisser kashai na mkuu wa wilaya ya kibondo venance mwamoto katika
hifadhi hiyo na vijiji vya kagoti, kumhasha na nduta ambapo kamanda
kashai amesema jeshi la polisi litawasaka wamiliki wa mashamba hayo
ambao walikimbia ili wafikishwe mahakamani.
Amesema watu wote waliokimbia
watasakwa na kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayowakabili ambapo
amesema oparesheni hiyo sasa ni endelevu na kwamba wameshapewa taarifa
na raia wema juu ya uwepo wa mashamba zaidi ya bangi katika maeneo
tofauti wilayani humo.
kwa upande wake mkuu wa wilaya ya kibondo venance mwamoto amesema kilimo
cha bangi wilayani humo kimeshamiri na kwamba imekuwa ikisafirishwa
kwenda nchi jirani na mikoa mingine na hivyo kuongeza matumizi ya madawa
ya kulevya katika jamii kinyume cha sheria .
Mwamoto amesema karibu asilimia
sabini ya mashamba ya mazao mbalimbali yanayolimwa wilayani humo
yanachanganywa na bangi hali ambayo inakuwa ngumu lakini watafanya
oparesheni hiyo katika maneo yote na kuwakamata wahusika na kuwachukulia
hatua za kisheria .
Kutokana
na hiyo amewataka viongozi wa hifadhi ya Muyowosi kushughulikia ulinzi
wa hifadhi hiyo ambao sasa umegeuzwa kuwa mashamba ya bangi ili kwa
pamoja waweze kudhibiti kilimo cha bangi wilayani humo.
oparesheni hiyo pia iliwezesha
kukamatwa kwa raia wanane wa burundi ambao walikutwa mashambani
wakifanya kazi za vibarua , wakiwa wameingia nchini , kuishi na kufanya
kazi kinyume cha sheria .
Kaimu afisa uhamiaji wa wilaya ya
Kibondo Rogert Mbele amesema wilaya hiyo ina wahamiaji wengi toka nchi
jirani ya Burndi ambao wamekuwa wakiingia nchini na kuishi vijijini huku
wakifanya kazi za vibarua mashambani .
Amesema hali hiyo inatokana na
ukubwa wa mpaka na udhibiti mdogo uliopo katika eneo hilo la mpaka na
kwamba hali hiyo inachangiwa na raia wan chi hiyo kuyafahamu zaidi
mazingira ya Kigoma kutokana na kuishi kama wakimbizi kwa miaka kadhaa
nchini .
Mwisho
JAMBAZI SUGU MBARONI NA SHEHENA YA RISASI
Na Fadhili Abdallah,Kigoma
JESHI la
polisi mkoani Kigoma limemtia mbaroni mwenyekiti wa kijiji cha Kwaga wilaya ya
Kasulu mkoani hapa akihusishwa na uchochezi uliopelekea mauaji ya mwananchi
mmoja wa kijiji hicho.
Kamanda wa
polisi Mkoa kigoma, Fraiser Kashai alisema kuwa mwenyekiti huyo, Baraka
Christopher anahusishwa kuwashawishi wananhi wa kijiji hicho kuvamia makazi ya
Peter Lukaya ambapo walichoma moto nyumbani yake na kumuua wakimuhusisha na
kufanya vitendo vya kishirikina.
Sambamba na
mwenyekiti huyo Kamanda Kashai alisema kuwa pia polisi inawashikilia wananchi
wengine wawili, Ramadhani Mohamed na Revocatus Mpomongo wakihusishwa na mauaji
hayo.
Aidha baada
ya mauaji hayo yaliyotokea mwishoni mwa wiki iliyopita polisi wilaya ya Kasulu
ilianza kuendesha msako kijiji hapo kuwatafuta watuhumiwa wa mauaji hayo hali
iliyozua mtafaruku mzito kijijini hapo.
Wakati polisi
wakiendesha msako wa kuwatafuta wauaji wananchi wa kijiji hicho walilalamikia
vitendo vilivyokuwa vikifanywa na polisi ambapo wananchi hao walifanya
maandamano kupinga unyanyasaji wa polisi katika kamata kamata hiyo.
Mwandishi wa
habari hii alishuhudia wananchi waliozuia barabara ya Kigoma kwenda Kasulu kwa
kujaza mawe barabarani hali iliyolazimu polisi kutumia silaha za moto na mabomu
ya kutoa machozi kuwatawanya watu hao.
Wakiongea na
gazeti hili baadhi ya wananchi wa kijiji hicho ambao walihofia kutajwa majina
yao waliwashutumu polisi waliokuwa wakifanya msako wa kuwatafuta watuhumiwa kwa
kusema kuwa polisi hao walikuwa wakivamia makazi ya watuhumiwa na kupora mali.
Mmoja wa
watuhumiwa aliyetajwa kuhusika na kadhia hiyo ni mwalim, Grace Kingaru ambaye
katika msako huo alipoteza simu mbili na pesa kiasi cha shilingi 300,000 na
baadaye simu yake moja ilikamatwa ikiwa imetuma meseji ya matusi kwa mkuu wa
upelelezi wa mkoa kigoma.
Mwalim huyo
alikamatwa akituhumiwa kuhusika na kuchochea wananchi kufanya vurugu kupinga
vitendo vya unyanyasaji wa polisi vilivyopelekea uvunjifu wa amani na uharibifu
wa mali ambapo hivi sasa mwalim huyo yuko nje kwa dhamana.
Kamanda wa
polisi Mkoa Kigoma, Fraiser Kashai alisema kuwa si haki kwa wananchi kufanya
vurugu na kuharibu mali badala yake wanapaswa kutoa taarifa kwa jeshi la polisi
kama kuna vitendo kama hivyo.
Alisema
kamanda Kashai kuwa Mwenyekiti huyo wa kijiji na watu wengine wawili ambao
walikamatwa kuhusika na mauaji hayo wanatarajia kufikishwa mahakamani wakati
wowote upelelezi utakapokamilika.
Mwisho.
MTU mmoja
ambaye anasadikiwa kuwa ni jambazi sugu amekamatwa na polisi akiwa na risasi
1200 sa bunduki za SMG,G3 na SAR akiwa katika harakati za kuzisafirisha risasi
hizo kwenda kuziuza.
Akizungumza
na waandishi wa habari mjini Kigoma jana Kamanda wa polisi Mkoa Kigoma, Fraiser
Kashai alimtaja mtu huyo kwamba Mwanzo Wilson aliyejitambulisha kuwa ni mkulima
na mkazi wa kijiji cha Kitambuka wilaya ya Buhigwe mkoani hapa mpakani na nchi
jirani ya Burundi.
Kamanda
Kashai alisema kuwa kukamatwa kwa mtu huyo kunatokana na taarifa kutoka kwa
raia wema kuhusu kuwepo kwa mpango wa mtu huyo kuzisafirisha risasi hizo katika
mbinu ambayo ingewahadaa vyombo vya ulinzi na usalama kuweza kumkamata.
Ili kukwepa vizuizi vya vyombo vya ulinzi na
usalama Kamanda Kashai alisema kuwa mtuhumiwa huyo alizificha risasi hizo
katika dumu la mafuta ya maweze jambo ambalo lingekuwa taabu kwa polisi
kumtilia mashaka.
Baadhi ya
askari kituoni hapo waliweza kuwaonyesha waandishiwa habari picha mbalimbali za
miaka ya nyuma zikimuonyesha mtuhumiwa akiwa amekamatwa kwa tuhuma za ujambazi
na moja ya matukio yake ni wizi uliotokea katika benki moja jijini Dar es
Salaam miaka mitatu iliyopita.
Aidha katika
tukio lingine polisi inamtafuta Tanu Nyandila Mkulima na mkazi wa kijiji cha
Kagerankanda wilaya Kasulu baada ya kukimbia na kutelekeza bunduki mbili aina
ya gobore ambazo alikuwa akizitumia kwenye matukio ya uhalifu na uwindaji
haramu.
Kamanda wa
polisi mkoa Kigoma alisema kuwa polisi kwa kushirikiana na askari wa idara ya
wanyama pori wa pori la hifadhi la Muyowosi Kigosi walipata habari za kuwepo
kwa mtuhumiwa huyo hata hivyo kabla ya kumtia mbaroni mtuhumiwa alikimbia na
kutelekeza magobore hayo mawili.
Mwisho.
Friday, April 5, 2013
BILIONI 32 KUBORESHA HUDUMA ZA MAJI KIGOMA UJIJI
Na Fadhili
Abdallah,Kigoma
MAMLAKA ya
maji safi na maji taka Kigoma Ujiji (KUWASA) inatarajia kutumia kiasi cha
shilingi bilioni 32 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa kuboresha huduma za
maji katika manispaa ya kigoma Ujiji na vitongoji vyake.
Akizungumza
katika mkutano wa wadau wa maji wa manispaa ya kigoma Ujiji kwa ajili ya
kutambulisha mradi huo Msimamizi wa mradi huo, Alex Kaaya kutoka wizara ya maji
na umwagiliaji amesema kuwa mradi huo unapaswa kukamilika mwezi Machi mwaka
2015.
Kaaya
amesema kuwa mradi huo unatekelezwa kutokana na ruzuku iliyotolewa na jumuia ya
ulaya na Shirika la KFW la Ujerumani
kwamba kutokana na kutolewa kwa fedha zote za mradi wanatarajia mradi
utakamilika katika muda uliopangwa.
Kwa upande
wake Mkurugenzi Mtendaji wa mamlaka ya maji safi na maji taka Kigoma Ujiji,
Simon Rutuga amesema kuwa sehemu kubwa ya utekelezaji wa mradi itajikita katika
kuanzisha chanzo kipya, ujenzi wa matanki ya kuhifadhia maji na usambazaji wa
mtandao mpya wa maji kwa urefu wa kilometa 70 kuhakikisha maji yanafika kwa
wananchi.
Rutuga
alisema kuwa kutekelezwa kwa mradi huo kunalenga pamoja na kuboresha huduma za
maji katika manispaa hiyo lakini pia kuifanya mamlaka hiyo iwe na uwezo wa
kujitegemea kwa asilimia 100 na hilo litawezekana kwa wananchi kulipia bili zao
kwa wakati kulingana na kuridhika na huduma wanayopata.
Akifungua
mkutano huo Mkuu wa wilaya Kigoma, Ramadhani Maneno amewataka wanasiasa
kusaidia kuweka utashi wao katika kuufanya mradi kukamilika kwa wakati badala
ya kuingilia na kukwamisha utekelezaji wa mradi.
Maneno
alisema kuwa hivi sasa wananchi wamekuwa wakipiga kelele sana kutokana na
kushsngazwa kuona ziwa likiwa mita chache kutoka kwenye makazi yao lakini
huduma za maji zimekuwa na matatizo makubwa.
Mwisho.
JAMBAZI SUGU MBARONI NA SHEHENA YA RISASI
MTU mmoja
ambaye anasadikiwa kuwa ni jambazi sugu amekamatwa na polisi akiwa na risasi
1200 sa bunduki za SMG,G3 na SAR akiwa katika harakati za kuzisafirisha risasi
hizo kwenda kuziuza.
Akizungumza
na waandishi wa habari mjini Kigoma jana Kamanda wa polisi Mkoa Kigoma, Fraiser
Kashai alimtaja mtu huyo kwamba Mwanzo Wilson aliyejitambulisha kuwa ni mkulima
na mkazi wa kijiji cha Kitambuka wilaya ya Buhigwe mkoani hapa mpakani na nchi
jirani ya Burundi.
Kamanda
Kashai alisema kuwa kukamatwa kwa mtu huyo kunatokana na taarifa kutoka kwa
raia wema kuhusu kuwepo kwa mpango wa mtu huyo kuzisafirisha risasi hizo katika
mbinu ambayo ingewahadaa vyombo vya ulinzi na usalama kuweza kumkamata.
Ili kukwepa vizuizi vya vyombo vya ulinzi na
usalama Kamanda Kashai alisema kuwa mtuhumiwa huyo alizificha risasi hizo
katika dumu la mafuta ya maweze jambo ambalo lingekuwa taabu kwa polisi
kumtilia mashaka.
Baadhi ya
askari kituoni hapo waliweza kuwaonyesha waandishiwa habari picha mbalimbali za
miaka ya nyuma zikimuonyesha mtuhumiwa akiwa amekamatwa kwa tuhuma za ujambazi
na moja ya matukio yake ni wizi uliotokea katika benki moja jijini Dar es
Salaam miaka mitatu iliyopita.
Aidha katika
tukio lingine polisi inamtafuta Tanu Nyandila Mkulima na mkazi wa kijiji cha
Kagerankanda wilaya Kasulu baada ya kukimbia na kutelekeza bunduki mbili aina
ya gobore ambazo alikuwa akizitumia kwenye matukio ya uhalifu na uwindaji
haramu.
Kamanda wa
polisi mkoa Kigoma alisema kuwa polisi kwa kushirikiana na askari wa idara ya
wanyama pori wa pori la hifadhi la Muyowosi Kigosi walipata habari za kuwepo
kwa mtuhumiwa huyo hata hivyo kabla ya kumtia mbaroni mtuhumiwa alikimbia na
kutelekeza magobore hayo mawili.
Mwisho.
Kamanda wa polisi mkoa Kigoma Fraiser Kashai (kushoto) akionyesha kwa waandishi wa habari bunduki aina ya Gobore ambayo ilikamatwa katika msako wa polisi sambamba na risasi 1200 (Picha na Fadhili Abdallah)
Subscribe to:
Comments (Atom)









