Friday, February 8, 2013
Baadhi ya askari waliomaliza mafunzo ya kujitolea ya jeshi la kujenga taifa katika kambi ya JKT Burombola wilaya ya Kigoma wakiwa kwenye mazoezi ya kupita maeneo yenye vikwazo ili kumkaribia adui
Na Mwandishi wetu, Kigoma
JESHI la kujenga taifa kikosi cha 821 Burombola mkoani Kigoma imesema kuwa haitaweza kufikia malengo ya uzalishaji waliyowekewa na makao makuu ya jeshi kutokana na kukabiliwa na mtaji mdogo na uharibifu wa wadudu waharibifu.
Akizungumza katika mahojiano maalum na gazeti hili Mkuu wa kambi hiyo, Meja Valentine Mrosso alisema kuwa kambi yake haitaweza kufikia uzalishaji wa hekari 600 walizopewa kutokana na changamoto hizo.
Alisema kuwa tatizo la mtaji kifedha, uharibifu unaofanywa na mchwa katika shamba la mahindi umechangia kurudisha nyuma malengo yao ya uzalishaji na kwamba kwa mwaka huu kambi hiyo imeweza kulima hekari 350 pekee.
Aidha Meja Mrosso alisema kuwa kambi yake haipati pembejeo za ruzuku ambazo zinatolewa kwa wakulima vijijini na serikali ambapo wameiomba serikali kuwaingiza katika utaratibu wa kupata pembejeo za ruzuku jambo ambalo litachangia kuwafanya waongeze uzalishaji.
Kwa upande wake meneja kilimo wa kambi hiyo, Adam Minzi alisema kuwa pamoja na changamoto hizo zinazowakabili lakini wamejiwekea malengo ya kuhakikisha wanalima hadi kufikia hekari 1000 katika kipindi cha miaka miwili ijayo.
Minzi alisema kuwa tayari wameshatoa taarifa kwa idara ya kilimo ya halmashauri ya wilaya kigoma kuhusiana na tatizo la mchwa ambao wamekuwa wakishambulia mahindi yaliyoanza kukomaa na hivyo kurudisha nyuma malengo ya uzalishaji.
Akizungumzia tatizo hilo Mkuu wa wilaya kigoma, Ramadhani Maneno alisema kuwa pamoja na malengo yaliyowekwa ya kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo lakini pia kambi za JKT na magereza mkoani humo ni maeneo ambayo mkoa unatarajia yatachangia kuongeza uzalishaji katika utekelezaji wa mkakati wa kilimo kwanza.
Maneno alisema kuwa tayari ameshatoa maelekezo kwa idara ya kilimo ya halmashauri ya wilaya kigoma kulifanyia kazi tatizo la mchwa linaloikabili kambi hiyo ya Burombola ili kuweza kukabiliana na athari ambazo zitaweza kutokea.
Mwisho.
Thursday, December 20, 2012
WAWILI WAUAWA KWA WIZI WA MBUZI
Na Fadhili Abdallah,Kigoma
WATU wawili wakazi wa kijiji
Nyamtukuza wilaya ya kibondo mkoani Kigoma wameuawa baada ya kupigwa na
wananchi wenye hasira kali wakituhumiwa kuiba mbuzi wawili wenye thamani ya
shilingi 40,000.
Kamanda wa polisi mkoa Kigoma
Fraiser Kashai aliwataja watu hao waliouawa kuwa ni Nongo Bufinkri (36) na
Azimio Muhabwa ambao waliiba mbuzi mali ya Sibalina John na waliuawa juzi
majira ya mchana kijiji hapo.
Hata hivyo Kamanda Kashai alisema
kuwa hadi sasa hakuna mtu yeyote aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo ambapo
mtuhumiwa mmoja alifanikiwa kukimbia kabla ya wenzake kukutwa na mauti.
Katika tukio lingine kamanda huyo wa
polisi mkoa kigoma alisema kuwa mkulima mmoja mkazi wa kijiji cha Kazuramimba
Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma Stephano Muhunzi (70) aliuawa kwa kukatwa katwa
mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake baada ya kuvamiwa na watu wanaosadikiwa
kuwa ni mjambazi.
Alisema kuwa katika tukio hilo watu
watano walivamiwa nyumbani kwa marehemu majira ya mchana na baada ya kumjeruhi
vibaya mwilini waliondoka na kondoo sita wenye thamani ya shilingi 300,000.
Aidha hadi sasa hakuna mtu yeyote
ambaye amekamatwa akituhumiwa kuhusika na tukio hilo na kwamba juhudi za
kuwatafuta wauaji zinaendelea.
Katika hatua nyingine Kamanda wa
polisi mkoa kigoma, Fraiser Kashai amewataka wananchi mkoani Kigoma kujihadhari
na watu wasiowema amabo wanafika kwenye makazi yao na kuwataka kutoa taarifa
kwa vyombo vya ulinzi na usalama wanapohisi kuna kitu cha namna hiyo.
Pia kamanda huyo wa polisi mkoa
kigoma amesema kuwa jeshi lake limejipanga vizuri kuhakikisha kwamba kuna na
amani na usalama wakati wote wa kipindi cha sikukuu za Christmas na mwaka mpya.
Mwisho.
RUN WAY AIRPORT KIGOMA
sehemu ya uwanja wa ndege Kigoma ambayo hivi sasa iko chini ya matengenezo kwa ajili ya kuifanya njia hiyo ya kurukia ndege kuwa ya kiwango cha lami
UKAGUZI UWANJA WA NDEGE KIGOMA
Waziri wa uchukuzi Dk.Harison Mwakyembe katikati akitembelea na kukagua matengenezo ya njia ya kurukia ndege kwa kiwango cha lami katika uwanja wa ndege wa Kigoma (wa kwa kulia) ni Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka ya hali ya hewa nchini, Dk.Agnes Kijazi.
Na Mwajabu Kigaza,Kigoma
WAZIRI wa
uchukuzi Harison Mwakyembe ameitaka mamlaka ya viwanja vya ndege nchini
kuhakikisha wananchi wa manispaa ya Kigoma ambao wanatakiwa kuhama kupishwa
upanuzi wa uwanja wa ndege wa Kigoma wanalipwa katika kipindi kifupi kijacho.
Akizungumza
muda mfupi baada ya kutembelea na kukagua maendeleo ya awamu ya kwanza ya mradi
wa ujenzi wa uwanja huo ambao unahusisha matengenezo ya njia ya kurukia ndege
kwa kiwango cha lami Mwakyembe alisema
kuwa hataki kusikia suala la fidia linakwamisha awamu ya pili ya upanuzi wa
uwanja huo.
Akizungumza
na viongozi na wafanyakazi wa idara mbalimbali katika uwanja wa ndege wa Kigoma
Waziri Mwakyembe alisema kuwa ni lazima hadi kufikia mwezi Februari mwaka ujao
wakazi hao wawe wameshalipwa na mwezi Julai awamu ya pili ya uwanja huo iweze
kuanza
Katika awamu
ya kwanza ya mradi huo inahusisha ujenzi wa mita 1800 ya njia ya kurukia ndege
kwa kiwango cha lami huku awamu ya pili ikihusisha kuendeleza urefu huo na
kufikia mita 3100 ambazo zitawezesha ndege aina ya Boing 737 na air Bus kutua
sambamba na ujenzi wa majengo mbalimbali uwanjani hapo ikiwemo jengo la kisasa
la abiria.
Aidha pamoja
na hatua nyingine Waziri huyo amesema kuwa ameridhishwa na kazi ya ukarabati wa
uwanja wa ndege wa kigoma inayofanywa na kampuni ya Syno Hydro ya China ambapo
ameitaka kampuni kuhakikisha kwamba uwanja huo unafunguliwa katika kipindi
kifupi kijacho ili kutoa nafuu ya usafiri wa ndege kwa wakazi wa mikoa ya
Magharibi.
Alikusema
kuwa kampuni hiyo imejenga imani kubwa
kwa serikali katika kuhakikisha inapewa awamu ya pili ya mradi wa ujenzi wa uwanja huo
kufikia hadhi ya uwanja wa ndege wa
kimataifa.
Akizungumzia
maendeleo ya ujenzi wa uwanja huo mhandisi mshauri wa mradi huo kutoka kampuni
ya stewart Scot International ya Afrika
Kusini , Cleopa Mpembeni amesema kuwa kumekuwa na maendeleo mazuri ya mradi huo
katika awamu hii ya kwanza na kwamba matarajio
na kuhakikisha ujenzi huo unaisha kufikia mwezi Februari mwaka ujao.
Mpembeni
alisema kuwa changamoto kubwa ambayo imekuwa ikiwakabili kwwa sasa ni kunyesha
kwa mvua nyingi mkoani kigoma jambo ambalo limesababisha wakati mwingine
kusimamisha kazi kwa siku nzima au
kufanya kazi hiyo nyakati za usiku.
Mwisho.
KUTUNUKU VYETI CHUO CHA HALI YA HEWA KIGOMA
Waziri wa uchukuzi Harison Mwakyembe (wa pili kushoto) akitunuku cheti
kwa amina Hussein (kulia) mmoja wa wahitimu 28 wa Diploma ya hali ya
hewa wakati wa mahafali ya chuo cha hali ya hewa mjini Kigoma kwa mwaka huu 2012
(picha na Fadhili Abdallah)
Waziri wa
uchukuzi Harison Mwakyembe ameiagiza mamlaka ya hali ya hewa nchini( TMA)
kufanya utafiti na kuon namna gani wanaweza kuwasaidia wananchi kukabiliana
radi zinazotokea na kuwadhulu watu wengi nchini kila siku.
Akizungumza
katika mahafali ya kuwatunuku vyeti wahitimu wa mafunzo ya diploma ya hali ya
hewa katika chuo cha hali ya hewa kigoma Mwakyembe alisema kuwa n lazima
wahitimu waonyeshe umahiri wao katika kuwasaidia wananchi kutokana na taaluma
wanayopata.
Aalisema kuwa
idara ya hali ya hewa imekuwa na umuhimu mkubwa kwa maisha ya wananchi lakini
umuhimu huo usiishie kwenye utabiri tu lazima wasomi wanaohitimu mafunzo katika
vyuo vya hali ya hewa ndani na nje ya nchi kuwasaidia wananchi kuona namna gani
tenkolojia ya kukabiliana na radi inaweza kuwasaidia wananchi.
Aidha sambamba
na hilo waziri huyo wa uchukuzi alisema kuwa mamlaka haina budi kurahisisha
utabiri wa hali ya hewa na kuufanya uwe na manufaa ya moja kwa moja kwa
mwananchi ili jamii na taifa liweze kupanga mipango yake kwa kuzingatia utabiri
unaotolewa na idara hiyo.
Waziri Mwakyembe
alisema kuwa ili kwenda na wakati na wananchi waone umuhimu wa uwepo wa taasisi
hiyo ni budi TMA ianze kutoa utabiri wa hali ya hewa kwa maeneo
madogo pamoja na elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa utabiri wa hali ya hewa.
kwa upande wake
mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya hali ya hewa nchini,Dk.A gnes kijazi amesema
katika kuboresha shughuli za mamlaka , wako katika hatua za mwisho kwa
kushirikiana na chuo kikuu cha Dar es salaam kuanza kutoa shahada ya hali ya
hewa.
Dk.Kijazi
alisema kuwa hata hivyo ufinyu wa bajeti umekuwa ukikwaza utekelezaji wa
mipango mbalimbali ya kimaendeleo ya mamlka hiyo na kwamba kwa mwaka ujao
serikali imeahidi kuiongeza bajeti mamlaka hiyo ili iweze kutekeleza mipango
yake kwa manufaa ya nchi.
kwa upande wao
wahitimu wa mafunzo hayo , pamoja na kuelezea matumaini yao baada ya kumaliza
masomo , wameiomba serikali kuyapatia ufumbuzi matatizo ya maabara, vitabu,
majengo na usafiri yanayokikabili chuo hicho pekee cha hali ya hewa nchini.
Mmoja wa
wahitimu hao, Shaban Dilunga akisoma
risala kwa niaba ya wajitimu hao alisema kuwa pamoja na changamoto hizo lakini
ufinyu wa bajeti na uchache wa fedha wanazipowa umechangia kuwafanya washindwe
kufanya mafunzo kwa vitendo (Field na study tour).
mwisho
KUHITIMU MAFUNZO YA MGAMBO
MKUU wa mkoa Kigoma Issa Machibya amewataka wahitimu wa kozi
ya mgambo kuzingatia nidhamu na kutumia mafunzo hayo kwa ajili ya kusaidia
shughuli mbalimbali za kijamii badala ya kuwa chanzo cha kuwaingiza kwenye
vitendo vya kihalifu.
Machibya alisema hayo katika hotuba iliyotolewa kwa niaba
yake na Mkuu wa wilaya Kigoma, Ramadhani Maneno wakati wa kufunga mafunzo ya
mgambo kwa watumishi 168 wa serikali mkoani Kigoma yaliyoenda sambamba na
maadhimisho ya miaka 51 ya uhuru.
Mkuu huyo wa mkoa amesema kuwa serikali ya mkoa imeamua
kufanyika kwa mafunzo hayo lengo likiwa kuwajengea ukakamavu watumishi wake
lakini pia kuongeza uzalendo miongoni mwa watumishi wake hasa vijan ambao
wameanza kazi miaka ya hivi karibuni.
Awali katika risala ya wahitimu hao iliyosomwa kwa niaba yao
na Noel Byamungu wamesema kuwa kumekuwa wamekuwambana na changamoto mbalimbali katika
mafunzo hayo ikiwemo kitendo cha mwajiri kushindwa kuwalipa stahili zao kwa
wakati.
Byamungu alisema kuwa kitendo kimechangia kuwafanya washiriki kutoshiriki mafunzo kwa
uhuru lakini kwani kimekuwa kikiharibu bajeti zao ambapo wameahidi kwamba
watatumia mafunzo hayo kwa kadri ya kiapo walichokula kwa maslahi ya Watanzania
wote.
Mwisho.
MSAADA WA BAISKELI KWA WATOA HUDUMA MAUMBANI
Mkuu wa wilaya Kasulu Dahn Makanga akimkabidhi baiskeli Thecla
Mtereke mmoja wa watoa huduma kwa wagonjwa wa ukimwi majumbani na magonjwa sugu ili kuwawezesha watoa huduma hao kufanya kazi zao kwa urahisi anayeshuhhudia ni Sister Philipina Rubavu, Katibu Mtendaji wa idara ya afya jimbo Katoliki Kigoma
KANISA
katoliki jimbo la kigoma limekabidhi baiskeli 88 zenye thamani ya shilingi
milioni 15 kwa watoa huduma kwa wagonjwa wa ukimwi majumbani wilayani Kasulu ili
kuwawezesha kuzitumia baiskeli hizo kurahisisha mawasiliano kati yao na
wagonjwa wanaowahudumia.
Baiskeli
hizo zilikabidhiwa kwa Mkuu wa wilaya kigoma, Dahn Makanga na Katibu Mtendaji
wa idara ya afya jimbo Katoliki, Philipina Rubavu ambapo naye Mkuu wa wilaya
Kasulu alikabidhi baiskeli hizo kwa watoa huduma 25 kwaniba ya watoa huduma
wengine katika hafla iliyofanyika mjini Kasulu mwishoni mwa wiki iliyopita
Akikabidhi
baiskeli hizo kwa watoa huduma Mkuu wa wilaya Kasulu, Dahn Makanga amewataka
watoa huduma hao kuzitumia baiskeli hizo kuwafikia wagonjwa na kuwapatia msaada
wanaohitaji.
Makanga
alisema kuwa ni wazi kazi wanayofanya watoa huduma hao ni kubwa na hailingani
na kiwango cha posho wanachopewa kwa kuwa wamekubali kujitoa na kwamba baiskeli
hizo ziwe motisha kwao kupunguza adha kutembea umbali mrefu kuwafuata wagonjwa
na kuwapatia huduma.
Naye
Philipina Rubavu, Katibu Mtendaji wa idara ya afya jimbo Katoliki Kigoma
alisema kuwa msaada huo umetolewa kupitia Tanzania Interfaith Partnership iliyo
chini ya Tume ya Taifa ya kudhibiti ukimiw nchini (TACAIDS).
Alisema kuwa
pamoja na changamoto mbalimbali watoa huduma hao ambao pia wanajishughulisha na
kuhudumia watoto wanaoishi katika mazingira magumu wamekuwa na changamoto kubwa
ya kufika maeneo mbalimbali.
Alisema kuwa
watoa huduma hao wanawahudhumia wagonjwa wa ukimwi wanaougulia majumbani na
wagonjwa wengine zaidi ya 400 na watoto wanaoishi katika mazingira magumu zaidi
ya 1000 wakifanya kazi katika vijiji zaidi ya 25 wilayani humo.
Wakizungumzia
msaada huo baadhi ya watoa huduma hao
walisema kuwa imekuwa faraja kubwa kwao kupata usafiri huo ambao utapunguza kwa
kiasi changamoto ya usafiri wa kufikia maeneo mbalimbali ya utoaji huduma
iliyokuwa ikiwakabili.
Thecla
Mtereke na Laurian Ntamahurilo alisema kuwa kabla ya kupata baiskeli hizo
walikuwa wakipata adha kubwa ya kutembea kwa mguu umbali mrefu kutoka eneo moja
kwenda eneo lingine kwa ajili ya kuwafuata wagonjwa wanaowahudhumia.
Mwisho.
Subscribe to:
Comments (Atom)